Ukamilishaji wa tamko la mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu pamoja na picha: Namna gani wamekamilisha utambuzi wa tatizo? Kitu gani kinafanywa na jopo la wataalamu walio kwenda kusaidia kuondoa tatizo la maji ya kunywa katika mji wa Basra kwa agizo la Marjaiyya?

Maoni katika picha
Baada ya mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi kuzungumza katika luninga (tv) asubuhi ya Ijumaa (07/09/2018m) ambapo aliongea kuhusu kuagizwa kwake na Marjaa Dini mkuu kuja kushughulikia tatizo la maji ya kunywa katika mji wa Basra, leo mtandao wa kimataifa Alkafeel unaeleza kwa urefu hatua na kazi zinazo fanywa na jopo la wataalamu katika kusaidia kuondoa tatizo la maji.

Muhandisi Dhiyau Majidi mmoja wa watalamu waliofuatana na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu amesema kua: “Kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu tumeanza kutekeleza hatua za kwanza za kurudisha maji safi na salama katika mji wa Basra kupitia kituo cha Albid’ah kinacho towa maji katika mto wa Ghuraaf, utendaji wa kazi unaendelea vizuri tukiwa na nyenzo zote za nguvu kazi na vifaa kwa ajili ya kufanikisha kazi hii, chini ya usimamizi wa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu na kwa kufuata maelekezo ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu huku tukiwa na matarajio ya kumaliza kazi haraka iwezekanavyo na kwa ubora mkubwa”.

Akaongeza kua: “Tulipo wasili katika mkoa huu, tulifanya vikao na viongozi wahusika, kisha tukaenda katika kituo cha maji cha Abbasi (a.s), kwa ajili ya kuchunguza tatizo na kuweka mikakati ya kulitatua, baada ya kufanya upembuzi yakinifu katika kituo hicho na kukagua mashine zake za kusukuma maji chini ya usimamizi wa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tukagungua kua kituo kilikua kimetelekezwa kwa muda mrefu, na kinafanya kazi chini ya kiwango, utendaji wake ni kati ya (%30-50), baadhi ya mashine hazifanyi kazi kwa sababu ndogo sana, kukosekana mtu wa kubadilisha kifaa kidogo tu”.

Akabainisha kua: “Kuna matatizo makubwa ya aina matatu:

  1. Kituo cha Abbasi (a.s) kinacho peleka kaji katika mradi wa Albid’ah kina mashine kubwa za kusukuma maji (32), mashine mbovu ambazo hazifai kutengenezwa tena na zinatakiwa kubadilishwa zipo (18) na zilizo baki; imma ni mbovu hazifanyi kazi na zinazo fanya kazi zinafanya chini ya kiwango.
  2. Hodhi la maji yanayo pelekwa katika mradi wa Albid’ah ni dogo.
  3. Mabomba yanayo peleka maji mjini ni mapovu na mengine yamepasuka.

Baada ya kubaini matatizo haya, tuliingia katika vikao vya kutafuta ufumbuzi wa haraka wa mambo hayo matatu yote yafanyiwe kazi kwa pamoja ili kufupisha muda wa kupatikana maji kwa watu wa Basra na kuondoa vikwazo vyote:

  1. Mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi alikutana na waziri wa maji pamoja na viongozi wa wizara hiyo kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo haya, wakakubaliana kuongeza ukubwa wa hodhi la maji yanayo kwenda katika kituo (mradi) wa Albid’ah liwe na urefu wa kwenda juu kati ya mita 5 hadi 7, ukubwa huo utatosha kusambaza maji kwa watu milioni 3 wakazi wa mji wa Basra kwa mujibu wa takwimu za idara ya maji ya Basra, na tunatarajia kuongeza urehu wa hodhi hilo hadi mita 9 siku za mbele kisha litaongezwa hadi mita 10 inshaallah.
  2. Sayyid Swafi aliagiza kuwasiliana na kufanya makubaliano moja kwa moja na shirika la (Caprari) ambalo ni shirika la kiiraq kwa ajili ya kuagiza mashine mpya za kusukuma maji zipatazo 18, ili ziondolewe zile zilizo kufa na kufungwa mpya, ndani ya muda mfupi mashine zote zitafanya kazi kwa uwezo wake wote, hadi sasa zimesha fungwa mashine mpya 8 kubwa zilizo nunuliwa mikoa tofauti ya Iraq, (Bagdad na mikoa ya kaskazini ya Iraq), kutokana na uhaba wa aina hiyo ya mashine na uchache wa kuhitajika kwake kwa matumizi madogo, tumewasiliana na watu mbalimbali hadi kupata mashine hizo, na zilizo baki zitaletwa. Pia tumetengeneza mashine zilizo kua mbovu na tumeongeza uwezo wa zile zilizo kua zinafanya kazi kwa kubadilisha baadhi ya vifaa na kuzifanyia matengenezo.
  3. Sayyid Ahmadi Swafi alimpigia simu waziri wa mafuta mara tatu na akakutana na mwakilishi wa waziri wa mafuta pamoja na baadhi ya viongozi wa wizara hiyo, sambamba na viongozi wa mashirika ya mafuta mara sita, kwa ajili ya kujadili utatuzi wa tatizo la tatu, baada ya vikao vivyo wizara imekubali kubeba jukumu la kuweka mtandao wa mabomba ya maji na kuondoa usumbufu wowote kwa wakazi, na kusambaza mabomba ya maji kwa wakazi wa Basra, kazi hiyo ikamilike sambamba na kukamilika kwa kituo cha maji, ili isitokee kufurika maji katika kituo cha Abbasi (a.s) pamoja na kuandaa kituo cha Dhwakh ambacho ndio kituo kikuu kinacho tumika kusambaza maji asilia na mazuri katika mkoa wa Basra. Baada ya makubaliano hayo wizara ilionyesha uwezo wake kwa kuanza kufanya kazi pamoja na wataalamu waliokuja na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu, na walianza kazi rasmi asubuhi ya Ijumaa katika sekta 4 (Makenika, Umeme, Uangalizi na Mitambo) kila sekta ikisimamiwa na wahandisi wawili, Muhandisi mmoja kutoka wizarani na mwingine kutoka katika jopo la ujumbe wa Marjaiyya”.

Naye mjumbe wa jopo la wataalamu katika ugeni wa Marjaiyya amebainisha kua: “Tumefanya kazi ya kusafisha na kutengeneza mahodhi ya maji yaliyopo katika vituo pamoja na kubadilisha vifaa vilivyo vimeharibika”.

Akasisitiza kua: “Kazi zote hizi zimefanyika ndani ya siku sita (6) tangu kuanza kwa utekelezaji wa agizo la Marjaiyya (2/9/2018m) tutaendelea kukujulisheni maendeleo ya kazi hadi mwisho kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu siku zijazo”.

Tunapenda kukumbusha kua baada ya kutokea tatizo la ukosefu wa maji safi na salama katika mkoa wa Basra, Marjaa Dini mkuu katika mkoa wa Najafu Ashrafu alituma ujumbe ukiongozwa na mwakilishi wake Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi akiwa pamoja na jopo la wataalamu kwa ajili ya kutafuta ufumbizi wa tatizo hilo wa haraka, wa muda wa kati na muda mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: