Kutokana na utangulizi huo, mafundi wa idara ya ushonaji ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamekamilisha kazi ya kushona bendera ya kubba tukufu itakayo pandishwa usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam (1440h) baada ya swala ya Maghribi na Isha katika kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo ni sehemu ya kazi zake rasmi, upandishaji wa bendera hiyo ni tangazo la kuanza mwezi wa Muharam mwezi wa huzuni.
Kiongozi wa idara Ustadh Abduzahara Daud Salmaan amezungumzia swala hili kua: “Kazi ya kusanifu na kushona bendera hupitia hatua kadhaa, kuanzia kuchagua aina ya kitambaa, ambacho kinatakiwa kua kitambaa imara kinacho weza kuvumilia mazingira ya hali ya hewa bila kufifia rangi yake, na kuchukua vipimo maalumu vya bendera kisha tunaingia katika kazi ya ushonaji, miongoni mwa wasifu wake ni:
- - Imetengenezwa kutokana na kitambaa bora na imeshonwa na kudariziwa kwa umaridadi wa hali ya juu.
- - Inaukumbwa wa mita tatu na nusu (3,5) upana na mita mbili na nusu (2,5) urefu.
- - Inapande mbili mfanano, kila upande umeandikwa neno lenye uhusiano na mwezi wa Muharam lisemalo (Ewe mnyweshaji wenye kiu Karbala) kwa hati ya thuluth, na kwa kalamu ya mtaalamu wa hati Ustadh Farasi Asadi, eneo la maandishi linaukubwa wa (1,2) mita moja na sentimita ishirini, na ukubwa wote jumla ni (2,5) mita mbili na nusu katika eneo lote la bendera na yameandikwa kwa rangi nyekundu.
- - Inauzito wa (2,5) kilo mbili na nusu takriban.
Kumbuka kua bendera hii itapandishwa usiku wa kwanza wa mwezi wa Muharam (1440h) baada ya swala ya Magharibi na Isha katika kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) kama tangazo la kuanza kwa maombolezo ya mwezi wa huzuni, bendera hiyo itapandishwa chini ya ratiba maalumu ya maombolezo ambayo hufanywa kila mwaka, Atabatu Abbasiyya tukufu imekua ikifanya hivyo tangu mwaka (2005m).