Katika msafara wa jopo la mafundi na wataalamu kwenye mji wa Basra: Kamanda wa polisi wa Basra na idara ya maji wanafanya kazi ya kuondoa vizuwizi katika vituo vya kusambaza maji ya Albid’ah…

Maoni katika picha
Baada ya mfululizo wa vikao vya mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu na jopo la wataalamu, pamoja na idara ya maji na kamanda wa polisi kila mmoja kwa nafasi yake, wamegundua kuwepo kwa vizuwizi vingi vya maji katika mashamba ya samaki yaliyo wekwa katika njia ya maji yanayo toka katika kituo cha Abbasi (a.s) kinacho endelea kutengenezwa na jopo la wataalamu miongoni mwa ugeni wa Marjaa Dini mkuu.

Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya mjumbe wa jopo la wataalamu Muhandisi Dhiyau Majidi, akaongeza kusema kua: “Hivyo! Ili wananchi waweze kunufaika na matengenezo yanayo fanywa na Marjaiyya, tumekubaliana idara ya maji ya Basra kwa kushirikiana na kamanda wa polisi waondoe vizuwizi katika njia ya maji”.

Mwandishi wa mtandao wa kimataifa Alkafeel alifuatana na kundi la waondoa vizuwizi katika mabomba ya maji kwenye kitongoji cha Baradwaiyya, kazi ambayo ilikua imesha wahi kufanywa na idara ya maji ya Basra katika kitongoji cha Ma’amil.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu alimuagiza mwakilishi wake Sayyid Ahmadi Swafi aende Barsa pamoja na jopo la wataalamu kwa ajili ya kutatua tatizo la maji safi ya kunywa, na kuweka mikakati ya kuondoa tatizo haraka na kuanza mora moja utekelezaji wake, utatuzi uwe wa haraka wa muda wa kati na wa muda mrefu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: