Maelekezo rasmi ya kitengo cha maadhimisho na Mawakibu pamoja na vikundi vya Husseiniyya katika kuhuisha maombolezo ya Ashura…

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na Mawakibu pamoja na vikundi wa Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimetoa maelekezo rasmi ya kuhuisha maombolezo ya Ashura, na imesisitiza umuhimu wa kuyatii, maelekezo hayo ni:

  • 1- Wajumbe wote wa Maukibu wanatakiwa kuswali mara tu baada ya adhana kila mmoja katika sehemu yake.
  • 2- Viongozi wote wa Mawakibu na vikundi vya Husseiniyya wanatakiwa kufuata maelekezo waliyo pewa na kitengo chetu, kuhusu nyakati za matembezi (masira) ya Mawakibu na vikundi vya (Zanjiil), ili kuzuwia msongamano katika matembezi yao.
  • 3- Kuheshimu maelekezo yote kutoka kwa watu wa usalama wanao husika na kitengo chetu, tusitowe mwanya kwa maadui wa Uislamu na maadui wa madhehebu ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).
  • 4- Msiruhusu kuingia watu msio wajua katika Maukibu yenu wakati wa matembezi (masira), nimarufuku kubeba siraha au kitu kinacho weza kujeruhi (kitu chenye ncha kali).
  • 5- Idara za Ataba mbili tukufu zinafuata maelekezo na ratiba inayo tolewa na kitengo chetu, mkuu wa Maukibu anatakiwa aonyeshe kitambulisho chake na utambulisho wa Maukibu kama tulivyo kubaliana wakati Maukibu yake itakapo karibia sehemu ya kuingia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
  • 6- Kiongozi wa Maukibu anawajibika kulinda usalama wa watu wake pamoja na vifaa vyao.
  • 7- Inaruhusiwa kuingia kamera moja tu pamoja na Maukibu na mbeba kamera avae kitambulisho chake.
  • 8- Tunatarajia wasomaji wa kaswida katika mimbari Husseiniyya ndani ya haram tukufu waheshimu muda walio pangiwa ambao ni (dakika kumi) hii inatokana na wingi wa Mawakibu na kuepusha msongamano.
  • 9- Tunatarajia Mawakibu zote na vikundi vya Zanjiil kuheshimu muda walio pangiwa kuwasili ambao ni kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa baada ya Adhuhuri, kwa sababu Mawakibu za matam zitaanza kuwasiri saa tisa baada ya Adhuhuri hadi katikati ya usiku.
  • 10- Hairuhusiwi kuingia na farasi ndani ya Ataba mbili tukufu kwa ajili ya kulinda usafi na utukufu wa maeneo haya.
  • 11- Baada ya adhana ya Adhuhuri ya siku ya kumu Muharam yataanza matembezi ya maombolezo ya Towarej.
  • 12- Vifaa vyote vya Maukibu viondolewe baada ya siku ya (13) ya mwezi huu wa Muharam.
  • 13- Likitokea tatizo (Alla atuepushie) watati wowote, tunatarajia watu wote wa Mawakibu muache barabara wazi kwa ajili ya kutowa nafasi kwa vyombo vya ulinzi na usalama.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: