Kukamilika kwa maandalizi ya kutangaza msimu wa huzuni na maombolezo katika Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imakamilisha maandalizi ya kutangaza msimu wa huzuni na maombolezo ya kumbukumbu ya kifo cha mjukuu wa Mtume na watu wa nyumbani kwake na maswahaba zake (a.s), itafanyika shughuli maalumu katika uwanja wa mbele ya mlango wa Kibla wa Abulfadhil Abbasi (a.s), shughuli hiyo itakua na vipengele vingi, kikiwemo kipengele cha kubadilisha bendera ya kubba tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s), ikitanguliwa na shughuli kama hiyo katika kaburi la ndugu yake Abu Abdillahi Hussein (a.s) ikihusisha kubadilisha bendera ya kubba lake tukufu kwa kushusha bendera nyekundu na kupandisha bendera ya huzuni na msiba ya rangi nyeusi.

Shughuli ya kupandisha bendera katika kubba la Abulfadhil Abbasi (a.s) itaambatana na mambo mengi, miongoni mwa mambo hayo ni; ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu na ujumbe kutoka kwa rais wa wakfu Shia na kukabidhi bendera kwa mmoja wa mikoa ya Iraq kisha kupandisha bendera nyeusi, na kubadilisha kwa ukamilifu bendera ya kubba tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhitimishwa kipengele hicho kwa kaswida ya kuomboleza.

Kwa upande mwingine Ataba mbili tukufu zimeshuhudia idadi kubwa ya mazuwaru waliokuja kushuhudia tukio hili huku vyombo vya usalama vikiwa vimeimarisha ulinzi.

Idara ya upigaji picha na uandaaji wa vipindi chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa masafa itakayo tumika kurusha matukio ya maombolezo ya Ashura ikiwa ni pamoja na tukio la kubadilisha bendera; inatoa fursa kwa vyombo vya habari kupokea matangazo kwa anuani zifuatazo:

SAT:INTELSAT 902@62°E
DL:11457.5V
SR:3000
DVBS2
8PSK
FEC 2/3
HD/MPEG-4
pamoja na matangazo ya moja kwa moja (mubashara) kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel ambao utarusha matukio hayo kama unavyo fanya katika matukio mengine kwa miaka mingi tena kwa upora wa hali ya juu.

Kumbuka kua shughuli hiyo na vikao vya taazia vimekua vikifanyika tangu mwaka (2004m), kupitia shuguli hiyo (ya kupandisha bendera) huwa ndio tangazo la kuingia mwezi wa huzuni, ambazo huanzia Karbala tukufu mji mkuu wa maadhimisho ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: