Kubadilisha bendera ya kubba la Imamu Hussein (a.s) na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoa za rangi nyekundu na kuweka za rangi nyeusi…

Maoni katika picha
Mwaka wa kumi na nne mfululizo baada ya swala ya Maghribi na Isha ya leo (30 Dhulhijja 1439h) sawa na (10 Septemba 2018m) umefanyika ubadilishaji wa bendera za kubba ya haram ya Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kutoa bendera nyekundu na kuweka nyeusi kama tangazo la kuingia mwezi wa Muharam 1440h.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wa dini na jamii pamoja na wafuasi wengi wa Ahlulbait (a.s) ambao wamejaa katika Ataba zote mbili na katika eneo la katikati ya Ataba hizo.

Ratiba ilianzia katika uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) na kufunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na bwana Osama Karbalai, kisha ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Husseiniyya ulio wasilishwa kwa niaba yake na makamo katibu mkuu wa utamaduni Sayyid Afdhalu Shami, ambaye alisisitiza sana vijana wajitolee kwa ajili ya kulinda mwenendo wa Imamu Hussein (a.s).

Akaongeza kua: “Kamilisheni jihadi yenu, imarisheni mapenzi yenu, dumisheni misimamo yenu kwa kulinda Dini yenu, mdumu katika swala na lindeni heshima ya wabawake wenu na malezi ya watoto wenu, wafundisheni adabu nzuri, lindeni umoja wenu na dumisheni safari ya islahi, wala msichoke au kuwa dhaifu mbele ya maadui na mbele ya mitihani pambaneni hadi mshinde, enyi ndugu zangu, enyi wafuasi wa Aali Muhammad enyi watoto wa Hussein, enyi wapenzi wa Imamu wa Zama hizi msiwaache maadui wakadhoofisha imani zenu, vumilieni matatizo ya njia ya islahi, na lindeni matunda ya jihadi yenu na kujitolea kwenu mliko fanya, hususan dhidi ya magaidi wa Daesh na dhidi ya mafisadi na waovu, msichoke kutafuta islahi na kubadilisha hali kuifanya iwe nzuri, hakika Mwenyezi Mungu ndio msaidizi wenu iwapo mtafanya subira na mkashikamana na misingi ya Imamu Hussein na watu wake watukufu (a.s)”.

Bendera nyukundu ikashushwa na kupandishwa bendera nyeusi, huku sauti zikisema (Labbaika yaa Hussein) kisha ikaimbwa kaswida ya kihistoria ya marehemu Shekh Haadi Karbalai katika kuupokea mwezi huu isemayo (Ewe mwezi wa Ashura) iliyo imbwa na mwimbaji mkubwa marehemu Hamza Zaghiir.

Baada ya hapo ikafuata shughuli ya kabadilisha bendera katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nako ratiba ilikuwa sawa na ile iliyo fanyika katika Atabatu Husseiniyya tukufu, ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya uliwasilishwa kwa niaba yake na Shekh Ali Mujaan, ambaye alisema kua: “Mwanzoni mwa Muharam Imamu Hussein huingia katika nyoyo za waumini na kulainisha roho zao, hakika huu ni msimu wa kulainika nyoyo, wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hupata faida nyingi sana kutokana na kumtembelea pamoja na kuhuisha maombolezo yake na kujitenga na maadui wake, nyie ni watoto wa wale walio katwa mikono yao kama gharama ya kuja kumtembelea (ziara), nyie ni watoto wa wale waliokua wanatembea usiku kuja ziara wakiogopa kukamatwa na matwaghuti, walifanya yote hayo kwa sababu kufika hapa ni kufuzu, (Hawawi sawa watu wa Motoni na watu wa Peponi. Watu wa Peponi ndio wenye kufuzu)”.

Akaongeza kua: “Enyi wahudhuruaji watukufu, hakika maadui wenu ambao hawatambui haki ya Imamu Hussein (a.s) bado wanaendelea kukufanyieni vitimbi na Mwenyezi Mungu ni mbora wa kulipiliza vitimbi, hakika nyie mpo katika heri kwa kuishi pamoja na Hussein, shuguli ya kubadilisha bendera ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ni tangazo la kuanza maisha mapya ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na Ahlulbait na Marjaa Dini wakuu, twaa ambayo tunaisoma kwa Abulfadhil (a.s)”.

Imekua ada tangu miaka kumi iliyo pita, kila mwaka hupokewa bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka katika moja ya mikoa ya Iraq, na mwaka huu ilikua zamu ya mkoa wa Diwaniyya, bendera hiyo ikapokelewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ikiwa katika jeneza, kisha ikashushwa bendera nyekungu na kupandishwa bendera nyeusi, shughuli ikafungwa kwa kaswida ya kuomboleza iliyo imbwa na Hussein Swagiir.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: