Ofisi ya wakili wa Marjaa Dini mkuu yakanusha taarifa aliyo nasibishwa nayo na yavitaka vyombo vya habari kuwa makini vinapo andika habari…

Maoni katika picha
Ofisi ya wakili (mwakilishi) wa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi imekanusha taarifa iliyo sambazwa na baadhi ya vyombo vya habari inayo sema kua “Mheshimiwa ametibua njama kubwa kwa watu wa Basra, ya kuzuwia kupatikana maji salama ya kunywa kwa wakazi wa mji huo”.

Akasisitiza kua: “Hakika habari hiyo sio sahihi, Sayyid Swafi hajaongea na chombo chochote cha habari zaidi ya taarifa aliyo ongea kwenye luninga (tv) siku ya Ijumaa (7/9/2018) ambayo alieleza jukumu alilo pewa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu”.

Ofisi imebainisha kua, Inakanusha habari zote zinazo nasibishwa na Mheshimiwa (Sayyid Swafi), habari hizo sio za kweli hata kidogo, habari sahihi ni zile zilizo andikwa na toghuti maalumu ya Atabatu Abbasiyya tukufu na zinazo fanana na hizo katika mitandao mingine.

Ikatoa wito: “Vyombo vyote vya habari kua makini na kuchukua tahadhari kwa kuandika habari kutoka katika chanzo chake rasmi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: