Barua kwa Imamu Hussein (a.s).

Maoni katika picha
Amma baad..

Zilikufikia barua kisha wakakugeuka baada ya kukwita, lakini barua za wafuasi wako zinatofautiana na za wale waliovunja ahadi zao, leo tunakuja kwako tukiwa kama ngao kwa ajili ya kuzuia mishale ya wale walio kufanyia hiyana, nakuandikia barua huku ukulele wa uhuru ukisikika hadi mbinguni, na minyororo ya utumwa inavunjika mbele yako pale ulipo kataa kujisalimisha, ukaandika ushindi kwa damu yako na utumishi mtukufu wa mikono miwili ya ndugu yako Abulfadhil Abbasi, na ukasambaza ushindi huo kupitia dada yako Aqiilat Zainabu, ukaenea kila pande ya Dunia na kuenea katika histozia milele, nani aliye huisha utukufu kama wewe ewe kiongozi wangu baada ya kudhalilishwa na mikono ya waovu walio mwaga damu ya watu wa nyumbani kwako.

Naomboleza kwa kukulilia, roho yangu ikutane na wewe ikilia kwa yaliyo kupata, mapenzi yangu kwako ni makubwa sana, nakulilia ewe bwana wangu nikiwa katika Dunia uliyo ikataa, hakuna maisha mazuri bila wewe ewe Abu Abdillahi, kwa nini isiwe hivyo wakati amesha sema kuhusu wewe Mtume Muhammad (s.a.w.w): (Imeandikwa katika nguzo ya Arshi: Hussein ni taa ya uongofu na safina ya uokozi), nisamehe nafsi yangu haiwezi kuandika baada ya kusikia wito wa Yaa Hussein, kutafuta katika lugha za Duniani maneno yafaayo kukuelezea haiwezekani (hayapo), wa mfano wako hawasifiwi (kwa ukamilifu) ispokua na viumbe wa mbinguni, kwa hiyo natosheka kwa kusema: Labbaika, nataraji uwe mwombezi wa kila atakaye soma barua yako siku ya ufufuo, na utuombee kwa Mwenyezi Mungu amlete haraka Imamu Mahdi Almuntadhir (a.f), jeraha lako haliponi kwetu hadi tulipize kisasi kwa maadui zako, na halita kamilika hilo ispokua kwa kuja Imamu Mahdi, Amani iwe juu yako siku uliyo zaliwa na siku uliyo uawa na siku utakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: