Kikosi cha wataalamu wa ugeni wa Marjaiyya chapata mafanikio zaidi na charusha ndege zisizo na rubani kugagua kazi.. na Sayyid Swafi awafananisha wanao zuia njia za maji sawa na (mdudu mnyonya damu)…

Maoni katika picha
Ofisi ya mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ahmadi Swafi imemuambia mtangazaji wa Somariya news katika mkoa wa Basra kua: “Ugeni wa Marjaiyya mkuu umeagizwa na Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Ali Husseini Sistani kuja kushughulikia tatizo la maji ya kunywa katika mkoa wa Basra, wanafanya kazi usiku na mchana, chini ya jopo la wataalamu waliokuja na Sayyid Swafi, wamepiga hatua kubwa katika kuondoa tatizo, baada ya siku chache walifanikiwa kufikisha maji katika baadhi ya mitaa ya Basra”.

Taarifa ikaongeza kua: “Sayyid Swafi alionyesha ulazima wa kuondoa vizuwizi katika njia za maji yatokayo katika kituo cha Abbasi (a.s) kwenda katika mradi wa Albid’ah, kwa sababu vizuwizi hivyo ni kinyume cha sheria za Iraq”.

Kiongozi wa ofisi ya Sayyid Swafi akasema kua watu wanao zuwia maji na kuyatumia wao ni sawa na: “Mdudu anaye ishi kwa kunywa damu za wengine, kwani wanachukua maji ambayo ni haki za watu wengine na ndio msingi wa maisha yao na uhai wao, halafu wanakuja kuwauzia kwa bei kubwa wakati ni haki yao waliyo ibiwa!!”.

Taarifa ikasisitiza kua: “Jopo la wataalamu chini ya amri ya Sayyid Swafi wamenunua mashine za kusukuma maji (20) kwa ajili ya mradi wa Albid’ah na wamepokea zawadi ya mashine mbili kutoka idara ya maji ya mkoa wa Karbala baada ya idara hiyo kutoa ushirikiano kwa jopo hilo”.

Taarifa ikasema kua: “Wataalamu hao walirusha ndege zisizokua na rubani kwa ajili ya kukagua kasi ya utokaji wa maji katika sehemu yaliyo kua yanatoka kidogo kidogo kutokana na vizuwizi vya maji vilivyo kuwepo katika mto wa Dujla”.

Ofisi ikabainisha kua: “Kiwango cha maji kinacho toka mto Dujla na kuelekea katika mji wa Qarna kimeongezeka katika siku za hivi karibuni, baada ya makubaliano yaliyo fikiwa katika vikao vya kikosi cha ugeni na wizara ya maji, vilivyo pitisha maamuzi ya kuondoa vizuwizi katika mto wa Dujla, jambo ambalo limesaidia kupunguza tatizo la maji kwa wakazi wa mji wa Qarna hadi nusu takriban”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: