Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu washirikiana na watu wa Tuuz katika huzuni zao wakati wa kupandisha bendera ya huzuni za Ashura…

Maoni katika picha
Ilipo ingia siku ya kwanza ya mwezi wa huzuni ya kifo cha Imamu Hussein (a.s), watu wa wilaya ya Tuuz ambayo ipo katika mkoa wa Swalahu Dini walipandisha bendera ya huzuni za Husseiniyya katika moja ya viwanja vya wilaya hiyo, shughuli hiyo ilifanyika mbele ya mwakilishi (mu’utamad) wa Marjaa Dini mkuu wa wilaya hiyo pamoja na wawakilishi wa vyombo vya ulinzi na usalama sambamba na watumishi wa mkoa, Atabatu Abbasiyya tukufu iliwakilishwa na watu kutoka kitengo chake cha dini, wakiongozwa na Sayyid Ali Yasiri kutoka katika kamati ya misaada ya kimkakati na muongozo ambayo ipo chini ya kitengo cha Dini, pamoja na kundi kubwa la wakazi wa wilaya hiyo.

Sayyid Yasiri alipata nafasi ya kuongea katika hafla hiyo, alitoa mkono wa pole kwa umma wa kiislamu na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kote Duniani kufuatia tukio hili baya lililo umiza roho ya Mtume (s.a.w.w), akasema kuwa bendera hii iwe kielelezo cha maneno ya bibi Zainabu (a.s), ya kwamba daima haki huwa juu na bendera itaendelea kupepea juu ya vichwa, na itakua taa kwa watu wa Tuuz linalo waangazia njia ya kufuata misingi ya mapambano ya Imamu Hussein (a.s), shughuli hiyo ilipambwa na majlis ya kuomboleza pamoja na baadhi ya kaswida na mashairi.

Kumbuka kua imekua desturi kupandisha pendera za huzuni ya Husseiniyya katika miji mingi ya Iraq na nje ya Iraq, kama alima ya kuanza kipindi cha huzuni za Husseiniyya na kuingia mwezi wa Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: