Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawaakibu Husseiniyya: Tumesajili zaidi ya Maukibu (elfu 29) kutoka ndani na nje ya Iraq (165) kutoka katika nchi za kiarabu na (22) kutoka katika nchi za kiajemi…

Maoni katika picha
Rais wa maadhimisho na mawaakibu Husseiniyya za Iraq na ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Idadi ya Maukibu na vikundi vya Husseiniyya vilivyo sajiliwa imezidi (elfu 29) vikiwa ni vya kuomboleza na kutoa huduma kutoka ndani na nje ya Iraq”.

Akaongeza kua: “Miongoni mwa majukumu ya kitengo chetu ni kuratibu utendaji wa mawaakibu Husseiniyya zinazo shiriki katika matukio mbalimbali yanayo hudhuriwa na mamilioni ya watu kama vile ziara ya Arubaini, kutokana na aina ya maukibu, kama ni maukibu ya kutoa huduma au maukibu ya kuomboleza, katika ziara ya Arubaini iliyo pita kulikua na maukibu zaidi ya (10,000), nchi za kigeni zilizo shiriki katika ziara hiyo zilikua (22) zikiwa na jumla ya maukibu (165), kitengo chetu kilitoa vitambulisho kwa mawaakibu zote na vilihifadhiwa katika ukurasa wa elektronik”.

Akabainisha kua: “Kitengo kimefanya juhudi kubwa, kimeteua wawakilishi katika mikoa mingi wapatao tisa, wanao simamia vikundi (160) vya Husseiniyya, wawakilishi hao walichaguliwa moja kwa moja na uongozi wa ndani ya kitengo, wawakilishi hao wamesaidia kupunguza matatizo ya pesa na kurahisisha mawasiliano baina ya kikundi na idara, wakati huo huo tumefanikiwa kuwa na uongozi mmoja wa mawaakibu katika kila mkoa, unao wajibika kuratibu maadhimisho kiofisi na kuwasiliana na serikali za maeneo husika baada ya kuwapa uwezo wawakilishi wa kufanya kazi na kuratibu maadhimisho katika kila mkoa”.

Akaongeza kua: “Hali kadhalika kitengo hiki kimetoa maelekezo kwa viongozi na wawakilishi wa mawaakibu na vikundi vya Husseiniyya ya kujiepusha na mambo ya vyama na siasa, washikamane na maelekezo ya Maraajii wakuu katika mji wa Najafu Ashrafu, tumeona wanatekeleza vizuri swala hili, pia kitengo kimeondoa baadhi ya vitendo vilivyo ingizwa katika maadhimisho ya Husseiniyya kama ilivyo elekezwa na Maraajii Dini wakuu katika mji wa Najafu Ashrafu, katika miaka ya hivi karibuni tumeshuhudia kuzuka mambo mengi katika maadhimisho ya Husseiniyya asilia”.

Akasisitiza kua: “Tulihimiza mawaakibu Husseiniyya ziitikie wito wa fatwa tukufu ya kujilinda kwa kuwasaidia wapiganaji na kufungua vituo vya kujitolea, walitoa misaada ya hali na mali kwa wapiganaji wa vikosi mbalimbali na katika hilo wakapatikana mashahidi na majeruhi wengi, pamoja na kushiriki kwao katika uwanja wa vita lakini pia walijitolea kuwahifadhi maelfu ya wakimbizi katika mawakibu na Husseiniyya zao”.

Akamaliza kwa kusema: “Kitengo cha maadhimisho kimekua msaada mkubwa katika sekta ya habari katika miaka ya hivi karibuni, kimewasaidia wanahabari kurusha matukio sahihi ya maadhimisho ya Husseiniyya kwa walimwengu, vituo vya luninga (tv) na mitandao ya kijamii ya kiislamu vimekua mstari wa mbele katika hilo, wanarusha habari za kila mimbari ya Husseiniyya, jambo ambalo limewavutia mamilioni ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na watu wengine katika kila kona ya Dunia, wanawasiliana nao na kuwafikishia ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) katika sura nzuri”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: