Wito mtukufu wa Husseiniyya wa Twafu na fatwa ya kujilinda...

Maoni katika picha
Baadhi ya watu wanaona kua tukio la Twafu (Karbala) la Imamu Hussein (a.s) ni tukio la kihistoria limesha pita na kuisha, haliwezi kuwa na athari yeyote baada ya kupita karne nyingi, mtazamo huo sio sahihi, mtu mwenye mtazamo huo hajui athari za uongozi kwa mwanadamu, wala hajui maana ya Hussein (a.s) wala maana ya kumnusuru, akili yake haiwezi kuchambua athari zilizo tokea katika historia, uongozi ni fikra, idikadi na malezi, uongozi wa Imamu Hussein (a.s) hauishii Twafu peke yake, upo katika mazingira ya kiroho ya Imamu Hussein (a.s) na namna alivyo fanya maandalizi ya hali ya juu katika harakati yake.

Tukio la Twafu linafundisha umoja wa jamii ulio onekana katika ardhi ya Karbala, iliyo beba misingi ya uminadamu na uzalendo.. watu wanao lelewa katika hali ya kujitolea lazima wawe wamoja na washikamane katika jambo lenye maslahi kwao, na katika jambo muhimu kwao, haya yalionekana pale sikika sauti ya Marjaa Dini mkuu ambaye ni kionganishi wa uongozi mtukufu wa Husseiniyya.

Marjaiyya tukufu ilikua inamiliki uwezo wa kuongoza watu kiroho, na vyombo vya habari –kwa miongo mingi- vimekua vikipuuza mambo ya kiroro, walifanya kila wawezalo kumsahaulisha mwanaadamu mambo ya kiroho, na kumuweka mbali na uongozi mtakatifu, hadi watu wakawa hawana hofu tena, viongozi wa Iraq wa serikali zilizo pita walifanya mambo makubwa yasiyo kua na uwadilifu wala huruma, wakadhofisha matumaini ya watu kwa viongozi, hadi raia wa Iraq akawa anaogopa madaraka, walifanya mambo kama yaliyo fanywa katika historia za kale, mateso kama hayo ndiyo waliyo fanyiwa wairaq, kama lilivyo undwa jeshi la Ibun Saadi, hivyo hivyo liliundwa jeshi la Daesh ili lije kufuta utajo wa Twafu na makaburi ya mawalii pamoja na kuwamaliza wafuasi wa Hussein (a.s).

Fatwa tukufu ya kujilinda ilikua na malengo makubwa miongoni mwa malengo ya Twafu ya Imamu Hussein (a.s), ya kurudisha uwelewa wa umoja wa kijamii, na kujenga moyo ya kujitolea, Imamu Hussein (a.s) alikuwa ndani ya fikra ya fatwa tukufu, na akaonesha uwepo wake katika mwitikio wa fatwa hiyo.

Fatwa ikawa jibu kali kwa mpango wa kurudisha utawala wa Umawiyya baada ya kutangaza kurudi kwao, wakiwa na chuki kubwa dhidi ya Ahlulbait (a.s), na kuja kufuta athari zote za Ashura, fatwa tukufu ikawa ni sauti ya Ashura inayo onyesha uwepo wa kizazi kinacho fuata mwenendo wa Imamu Hussein (a.s) wa islahi.

Walimwengu walipuuza mapambano ya Husseiniyya na wakatangaza kushindwa kwa fatwa tukufu; ili kuzuwia athari ya ushindi huo kwa walimwengu, hakika mapambano yalifanyika kwa umakini mkubwa na ubinaadamu wa hali ya juu, yalijenga moyo wa kujitolea, wapambanaji wakaendelea kupandisha bendera ya haki, na kujitolea zaidi kuvunja misingi ya matwaghuti, wananchi wakaitikia kwa wingi fatwa hiyo jambo lililo watisha watawala, fatwa ilikua tamko la kuwataka watu watende, wahurumiane na kuhuisha dhamira.. ikatupeleka katika msafara ya Hussein na harakati yake ya milele.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: