Atabatu Abbasiyya tukufu yaratibu majaalis za Husseiniyya…

Maoni katika picha
Bado zinaendelea kuonekana picha za maombolezo ya Husseiniyya katika mwezi wa Muharam na Safar kutokana na yaliyo msibu bwana wa mashahidi (a.s), macho hujaa machozi na nyoyo huhuzunika na kuugulia.. kutokana na msiba mkubwa ulio tetemesha ardhi na mbingu, Atabatu Abbasiyya tukufu kufuatia ratiba yake ya kuhuisha kumbukumbu ya muhanga wa Imamu Hussein (a.s), muhanga ambao ulibadilisha historia kwa damu kushinda upanga, imeratibu majaalisi za maombolezo ya Ashura ambayo ni moja na misingi muhimu ya kubakia kwa harakati hii, na sehemu ya kupata mafundisho mbalimbali na mazingatio, zimekua sawa na taa linalo waangazia wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s).

Majlis hizo zinafanyika kila siku ndani ya mwezi wa Muharam, zikihutubiwa na masayyid na mashekh kutoka katika kitengo cha Dini kwa nyakati na sehemu tofauti, kuna ambazo zinafanyika ndani ya uwanja wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), majlisi hizi hufanywa kila mwaka kwa muda wa siku kumi na tatu kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam, katika vipindi viwili, asubuhi na baada ya swala za Duhurain, kwa namna ambayo hazizuwii harakati za mawaakibu zinazo ingia katika uwanja wa haram tukufu, majlis hizo huhudhuriwa kwa wingi na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na mazuwaru, na huhitimishwa kwa matam ambayo huongozwa na mwimbaji Mulla Hamiid Tamimi ambaye huimba kaswida za ushairi zinazo elezea yaliyo jiri kwa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake (a.s) katika siku hizi.

Kuna majlis nyingine hufanywa ndani ya ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na watumishi pamoja na mazuwaru, pamoja na majlis nyingine ambayo hufanywa katika uwanja wa haram tukufu mbele ya mlango wa kitengo cha Dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya hufanya majaalis mbalimbali na hutoa mihadhara ya kifiqhi na kiaqida ambayo hulenga kuonyesha dhulma walizo fanyiwa Ahlulbait (a.s), pamoja na malengo na matokeo ya harakati tukufu ya Imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: