Uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) umetandikwa kapeti jekundi katika eneo la zaidi ya mita za mraba (10,000)…

Maoni katika picha
Kufuatia kukamilika maandalizi maalum ya ziara ya mwezi kumi Muharam ambayo humiminika kwa wingi mawaakibu za kuomboleza, na kwa ajili ya kuhifadhi miswala ya uwanja mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kurahisisha utembeaji wa mawaakibu na mazuwaru, kitengo cha uangalizi wa haram tukufu cha Atabatu Abbasiyya kimetandika kapeti jekundu katika uwanja wa haram tukufu katika eneo linalo kadiliwa kufikia mita za mraba (10,000).

Rais wa kitengo cha uangalizi wa haram Ustadh Hassan Hilali ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kutandika kapeti katika uwanja wa haram tukufu katika kipindi cha ziara ya Ashura ni miongoni mwa majukumu yetu, tulichukua vipimo vya eneo hili na tukachagua aina muwafaka ya kapeti, tumechagua aina ngumu ambayo sio laini yenye unene maalumu isiyo kua na utelezi na inauwezo mkubwa wa kushikamana na ardhi bila kuachia achia, kwa ajili ya kurahisisha utembeaji wa mazuwaru na mawaakibu za kuomboleza za Tuwareji”.

Akaongeza kua: “Kwa kusaidiana na baadhi ya vitengo vya Ataba tukufu, kikiwemo kitengo cha masayyid watumishi tumetandua miswala ya uwanja wa haram tukufu na kuipeleka stoo, kisha tukasafisha na kutandika nailoni nzito katika eneo la ukubwa wa mita za mraba (8,000), halafu tukatandika kapeti juu yake na kuambatanisha kapeti na nailoni hadi ikawa kama kitu kimoja, sehemu zilizo tandikwa ni uwanja wa haram tukufu na sehemu za korido na milangoni pamoja na eneo linazo zunguka kaburi tukufu la Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kua kitengo hiki –sawa na vitengo vingine vya Atabatu Abbasiyya tukufu- kinatumia uwezo wake wote kuwapokea waombolezaji na mawaakibu Husseiniyya, ambapo kilele chake ni mwezi kumu Muharam na hufanyika maombolezo ya tuwareji ambayo huhudhuriwa na mamilioni ya watu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: