Kufuatia mwezi wa Muharam Skaut ya Alkafeel yaendesha ratiba ya (Labbaika yaa Hussein)…

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa wanachama (300) wa Skaut, Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chini ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendesha ratiba ya pili ya wanaskaut iitwayo (Labbaika yaa Hussein), kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Muharam, nayo ni ratiba inayo husisha utowaji wa huduma, utamaduni (mafunzo) na habari, itachukua siku sita, kuanzia mwezi tatu Muharam hadi mwezi nane kwa muda wa saa kumi kila siku, na inahusisha vikosi vitatu vya Akaut ambavyo ni, kikosi cha Ashbaal cha vijana wenye umri wa miaka (9 hadi 12), kikosi cha Kashaafah cha vijana wenye umri wa miaka (13 hadi 15) na kikosi cha Jawwaalah cha vijana wenye umri wa miaka (16 hadi 18).

Kipindi cha asubuhi kuanzia saa mbili hadi saa saba Adhuhuri wanatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru, na kipindi cha jioni kuanzia saa saba hadi saa kumi na mbili Alasiri, wanagawa maji kwa mazuwaru pamoja na kuwapaka marashi na kuwaelekeza katika maeneo wanayo taka kuyazuru, vijana wa Skaut wamesambaa katika milango ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na ndani ya uwanja huo na wamekaa kwa vikundi.

Kuhusu upande wa malezi, washiriki wanapewa mafunzo ya kutoa mihadhara ya kidini kuhusu harakati ya Imamu Hussein (a.s) na tukio la Ashura, na kuhusu upande wa habari, wanafundishwa namna ya kutoa mihadhara inayo rushwa katika vyombo vya habari kulingana na umri wao kama walivyo fundishwa katika mafunzo ya Skaut hatua ya pili waliyo hitimu hivi karibuni.

Tariba hii inatekelezwa kwa kushirikiana na vitengo vingine, kikiwemo kitengo cha nidhamu, kitengo cha mawaakibu, kitengo cha uangalizi wa haram, kitengo cha utumishi, na kitengo cha mitambo.

Tunapenda kufahamisha kua jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imesha toa mafunzo mbalimbali na kutoa huduma tofauti ambazo zimesaidia kukuza uwezo wa vijana katika sekta tofauti zinazo jenga utu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: