Maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) katika macho ya waombolezaji wake na mawakibu zao zajikumbusha misimamo ya ushujaa katika vita ya Twafu…

Maoni katika picha
Maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) wanasifa za pekee kabisa zinazo wafanya kuwa mashahidi bora, watu hao walikua na uhusiano maalumu na Imamu wa zama zao Abu Abdillahi Hussein (a.s), walionyesha misimamo mbalimbali iliyo dhihirisha ukubwa wa utekelezaji wao wa sheria, ulio tokana na mapenzi yaliyo jengeka na kumtambua Imamu wa zama zao (a.s), Imamu Hussein (a.s) aliwasifu kwa kusema: (Mimi sijui maswahaba bora na waaminifu kushinda maswahaba wangu, na Ahlubait (ndugu) wema na wenye kuunga undugu kushinda Ahlulbait (ndugu) zangu).

Kutokana na jambo hilo mawaakibu za kuomboleza za watu wa Karbala zina utamaduni wa miaka mingi, wa kutenga siku maalumu ya kuwazungumzia answari wa Imamu Hussein (a.s) wakimtanguliza mzee wao Habibu bun Mudhwahir Asadiy, ambayo huwa ni usiku wa sita wa mwezi wa Muharam pamoja na mchana wake, sauti hupazwa, kaswida hutungwa, vifua hupigwa na mawaakibu hukumbuka msimamo wa kundi dogo la waumini walio simama pamoja na haki dhidi ya batili.

Kama kawaida mawaakibu huanza matembezi yao pembezoni mwa mji wa Karbala na huja moja kwa moja hadi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha huelekea kwa mkuu wa msiba Imamu Hussein (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya harama mbili tukufu, halafu hufanya majlis ya kuomboleza huko kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya usimamizi mkali wa vikosi vya usalama na watumishi, kwa ajili ya kuweka mazingira salama ya kuomboleza na kutembea kwa amani kwa mazuwaru na mawakibu zenyewe.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: