Maoni katika picha
filamu ya (bwana wa maji) inayo muhusu Abulfadhil Abbasi (a.s) matukio yaliyopo katika filamu hiyo yanaonyesha baadhi ya ushujaa na misimamo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu, na jinsi alivyo jitolea kwa ajili ya ndugu yake Imamu Hussein (a.s) na familia yake likiwemo tukio la kuwanywesha maji, filami hiyo imetengenezwa kwa ubora mkubwa, imewekwa vionjo vingi ikiwa ni pamoja na mambo ya kihistoria, uzungumzaji na watu walio shiriki katika kazi hiyo, pamoja na utaalamu wa hali ya juu uliopelekea kufaulu kwa kazi hii.
Kumbuka kua kazi hii tukufu ilipata zawadi ya ushindi wa kwanza katika mashindano ya filamu yaliyo fanyika katika kongamano la kimataifa la Ghadiir lililo fanyika siku za nyuma, nayo ni moja miongoni mwa kazi nyingi zilizo fanywa na studio chini ya wataalamu wake walio bobea katika sekta hiyo.