Hivi ndio zilivyo huisha mawaakibu za kuomboleza na kundi la mazuwaru usiku wa Abulfadhil Abbasi (a,s) –kwa picha-…

Maoni katika picha
Usiku na mchana wa saba katika mwezi mtukufu wa Muharam unafungamana na Abulfadhil Abbasi (a.s), wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na hasa hapa Iraq wamezowea kuomboleza siku za Ashura kwa kuipa kila siku muhusika maalumu miongoni mwa wale waliokua na nafasi kubwa katika vita ya Twafu, kwa ajili ya kuangazia zaidi msiba wa bwana wa Mashahidi Abu Abdillahi Hussien (a.s), msiba ulio waumiza sana viumbe wa nbinguni na ardhini, japo kua mauwaji yote yalitokea siku moja bali sehemu ya mchana wa mwezi kumi Muharam mwaka wa (61) hijiriyya.

Kwa hiyo katika usiku na mchana wa saba Muharam mawaakibu humuomboleza rasmi Abulfadhil Abbasi (a.s) mtoto wa Haidari Karraar na mbeba bendera ya Imamu Hussein (a.s) ambaye alionyesha ushujaa wa hali ya juu katika mapambano ya Twafu, na ambye katika msimamo wake kuna bahari ya masomo na mazingatio, miongoni mwa matukio aliyo fanya katika siku kama ya leo aliwapa maji watu wa Imamu Hussein na famalia yake, na ukaonekana ushujaa wake kupitia tukio hilo tukufu.

Kama kawaida mawaakibu huanzia metembezi yao pembezoni mwa mji wa Karbala na huja hadi katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kisha huelekea kwa muhusika mkuu wa msiba Imamu Hussein (a.s) wakipitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kisha hufanya majlis ya kuomboleza kwa kufuata ratiba iliyo andaliwa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kilicho chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya chini ya ulinzi mkali na huduma bora kutoka kwa watumishi wa Ataba, kwa ajili ya kutengeneza mazingira ya huzuni na kurahisisha matembezi ya mazuwaru na mawaakibu za kuomboleza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: