Mwezi saba Muharam: Mnyweshaji maji Abulfadhil Abbasi (a.s) avamia mto Furat na kuchota maji ya kunywa ndugu yake Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake…

Maoni katika picha
Riwaya mbalimbali zinasema kua: siku ya saba ya mwezi wa Muharam mwaka wa (61h) Abulfadhil Abbasi bapoja na baadhi ya maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) walipewa jukumu la kwenda kuvamia mto Furat na kuchota maji kwa ajili ya kunywa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake, wakachukua viriba (vyombo) vya kubebea maji (20) kwa ajili ya kuja kuwapa maji wale walio zidiwa na kiu.

Imepokewa kuwa; baada ya Imamu Hussein (a.s) na maswahaba zake kushikwa na kiu kali, alimwita ndugu yake Abbasi (a.s) akampa wapanda farasi thelathini na watembea kwa miguu ishirini wakiwa na viriba vya kuchotea maji ishirini katikati ya usiku, akaambia waende kuleta maji, wakaondoka kuelekea mtoni kuchota maji wakiwa wametanguliwa na Naafii bun Hilali Almuraadi aliye kuwa miongoni mwa wafuasi waaminifu wa Imamu Hussein (a.s), walipo karibia mtoni Omari bun Hajjaaj Zubaidi ambaye ni miongoni mwa waovu wa vita ya Karbala na aliye kuwa amepewa jukumu la kulinda mto wa Furat, akasema kumuambia Naafii: unakuja kufanya nini? Naafii akajibu, tumekuja kunywa maji mliyo tuharamishia. Omari bun Hajjaaj akasema: kunywa. Naafii akasema, Ninywe mimi wakati Hussein na watu wake wana kiu?! Omari akasema: hakuna ruhusa ya kuwapa maji ya kunywa watu hao, hakika sisi tumewekwa hapa kuzuwia wasipate maji. Watu wa Imamu Hussein (a.s) hawakujali maneno hayo, wakayadharau na wakavamia mto Furat na wakajaza maji katika viriba vyao, Omari bun Hajjaaj na jeshi lake likataka kwenda kuwazuwia wasichote maji, ndio Abulfadhil Abbasi (a.s) na Naafii bun Hilali, wakaanza kupambana na jeshi hilo, wakapigana vita kali sana lakini pande zote mbili hakuna aliye kufa, watu wa Imamu Hussein (a.s) wakarudi wakiwa wamejaza maji kwenye viriba vyao.

Kuanzia siku hiyo Abulfadhil Abbasi akapewa jila la “Saqaa” nalo ni jina (lakabu) maarufu sana, na tukufu zaidi kwake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: