Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wanamkumbuka bosi wao katika siku yake na wanaonyesha uwaminifu wao na kumuahidi kufuata nyayo zake na kuwahudumia mazuwaru wake…

Maoni katika picha
Sawa na mawakibu zingine za Karbala za kuomboleza msiba wa Imamu Hussein (a.s), watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya maombolezo rasmi katika siku inayo nasibishwa na jina lake, wametoka na kufanya matembezi ya kuomboleza wakiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar.

Matembezi hayo ya kuomboleza ambayo Ataba tukufu imekua ikiyafanya mara nyingi katika kumbukumbu za vifo vya Maimamu (a.s), walisimama kwa mistari kwa ajili ya kutoa pole mbele ya kaburi tukufu kwa maombolezo ya Ashura na kuuwawa kwa ndugu yake Imamu Hussein (a.s), kwa kusoma kaswida na mashairi yaliyo leta simanzi na majonzi makubwa, wakati huo huo wakaahidi kufuata nyayo zake na kutoa huduma bora kwa mazuwaru wake.

Baada ya kisimamo cha maombolezi kilicho onyesha kuenzi msimamo, uaminifu na ushujaa alio kuwa nao Abulfadhil Abbasi (a.s) katika vita ya Twafu ya milele, wakatembea kuelekea katika kaburi la mwenye msiba Abu Abdillahi Hussein (a.s), na wakafanya majlis ya kuomboleza huko pamoja na watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu sambamba na kusoma kaswida za kuomboleza na kupiga matam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: