Mheshimiwa Sayyid Swafi akiwa Basra: Baada ya kumaliza kazi yetu jopo la wataalamu nilio kuja nao watabaki hapa wakisimamia mafanikio haya kwa muda wa mwaka mmoja…

Maoni katika picha
Mjumbe wa Marjaa Dini mkuu katika mkoa wa Basra Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi ametangaza kukamilika kwa kazi aliyo pewa katika mkoa wa Basra.

Amebainisha mambo mengi yanayo husiana na kazi aliyo pewa na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Ayatullah Sayyid Sistani ya kwenda kutatua tatizo la mkoa huo, kupitia ujumbe aliotoa asubuhi ya Juma Tatu (7 Muharam 1440h) sawa na (17 Septemba 2018m) mambo muhimu aliyo sema ni:

 • 1- Jukumu tulilo pewa –kama tulivyo sema mwanzo- ni kushughulikia tatizo la maji safi ya kunywa katika mkoa kipenzi wa Basra.
 • 2- Baadhi ya matatizo hatuwezi kuyamaliza kwa siku kumi na tano, tatizo lililodumu miaka kumi na tano haliwezi kumalizwa kwa siku kumi na tano.
 • 3- Kwa masikitiko makubwa, mradi wa kituo bora cha maji ya kunywa ulio anzishwa mwaka 1997 haukuwa na uwangalizi wala haukutiliwa umuhimu, lau ungekamilika ungemaliza tatizo kwa kiasi kikubwa.
 • 4- Baada ya kubaini tatizo tulinunua mashine za kusukuma maji, hadi leo zinafanya kazi zaidi ya mashine ishirini na tano, tulinunua mashine ishirini na zingine tumepewa na wasamalia wema.
 • 5- Tumeondoa baadhi ya mashine za zamani na kufunga mashine mpya zenye upora mkubwa, na baadhi ya mashine za zamani zimerekebishwa na zinaendelea kufanya kazi.
 • 6- Kwa sasa mradi unaendelea vizuri sana, lakini haimanishi maji yamefika kwenye kila mtaa katika mkoa wa Basra.
 • 7- Tatizo ni kubwa, na sisi tumetekeleza jukumu letu ndani ya muda wa wiki mbili.
 • 8- Baadhi ya vyombo vya habari vilisema kuwa pesa iliyo tumika ni dinari mioni (50), habari hiyo sio sahihi pesa zilizo tumika ni nyingi sana zaidi ya hizo.
 • 9- Sababu ya kutofika maji katika kila mtaa wa Basra imetokana na matatizo yaliyo pandana, kuna mabomba yanayo peleka maji safi katika matavi ya vituo vya maji, kwa bahati mbaya mabomba hayo yamewekewa vizuwizi, maji yanayo zuwiwa katika kizuwizi kimoja yanatosha kuhudumia zaidi ya nyumba mia saba.
 • 10- Vizuwi vimejaa katika njia yote ya maji.
 • 11- Tumewapa jukumu watu maalumu wahakikishe wanaondoa vizuwizi vyote.
 • 12- Tatizo lingine ni vituo vilivyopo, nasema: kuna kazi nzuri inayo fanyika na kama ikiendelea tatizo litaisha.
 • 13- Sasa hivi maji safi ya kunywa yameanza kufika katika mitaa mingi na hayakatiki katiki.
 • 14- Jukumu langu nililo pewa nimelitimiza pamoja na wataalamu nilio kuja nao.
 • 15- Kuna baadhi ya mambo yanahusiana na vyombo vingine, haiwezekani kubeba matatizo ya watu wengine na hayapo katika jukumu letu.
 • 16- Inatakiwa vizuwizi vyote vya maji na viondolewe.
 • 17- Baadhi ya vyombo vilishirikiana vizuri na sisi na baadhi havikutoa ushirikiano kabisa kama vile jambo hili haliwahusu.
 • 18- Mamlaka zinazo husika na kuteua watumishi ziwe makini katika uteuzi wao na ziwajengee uzalendo.
 • 19- Mambo yaliyo tusukuma kuja kutatua tatizo la maji katika mji huu ni mambo mawili, pamoja na agizo la Mheshimiwa Sayyid Sistani, jambo la kwanza ni uwepo wa picha nyingi za mashahidi katika mji huu, ikawa kama vile mashahidi wanatuangalia na kututaka tusaidie familia zao.
 • 20- Jambo lapilli linatokana na aina ya tatizo, nalo ni tatizo la maji ambayo ni haki ya kawaida kwa kila mtu duniani, ukichukulia kuwa tupo katika mwezi wa Muharam sehemu ya maombolezo yetu yanahusu maji.
 • 21- Bila shaka mkoa wa Basra umedhulumiwa, na umefanyiwa dhulma nyingi sana, ni wajibu kwa watu wa mji huo na kwa uwezo wao waondoe dhulma, haifai kuishi katika dhulma milele.
 • 22- Inatakiwa ndugu zetu wana sheria wa Basra waibane serikali ili wapewe haki zao.
 • 23- Natarajia serikali iwe na uwelewa, jambo muhimu inatakiwa kuwapa haki zao raia wake.
 • 24- Sikupata jibu nilipo wauliza: je watu wa Basra mnawapa haki yao ya gawio la mauzo ya mafuta?
 • 25- Mimi naomba watu wawe siriasi watafanikiwa kutatua matatizo mengi.
 • 26- Tatizo lingine ni tatizo la usimamizi, kama idara ya maji ingetekeleza majukumu yake vizuri tatizo lisingekuwa kubwa kiasi hiki.
 • 27- Idara nzuri ni ile yenye usimamizi mzuri.
 • 28- Lazima kuwe na idara nzuri zenye utendaji mzuri katika serikali ya mkoa na serikali ya taifa itakayo ondoa ufisadi.
 • 29- Wataalamu tulio kuja nao watabaki hapa kwa muda wa mwaka mmoja kwa ajili ya kusimamia kazi tuliyo fanya katika siku hizi.
 • 30- Tumeanzisha mtandao wa kamera na tumepiga picha kwa juu na tumefika hadi kwenye chanzo cha mto Albid’ah.
 • 31- Natoa shukrani kwa kila aliye saidia na kushiriki pamoja nasi kwa njia yeyote ile katika kutatua tatizo hili.
 • 32- Hakika ilikua ni fursa tukufu sana kwetu ya kuwahudumia ndugu zetu wapenzi wakazi wa mji huu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awalinde.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: