- - Wakazi wa mkoa wa Karbala na mikoa ya kati na kusini, wakutane katika jengo la Imamu Askariy (hoteli ya Dalla ya zamani) iliyopo katika eneo la mlango wa Bagdadi baada ya Adhuhuri ya siku ya Juma Tano 9 Muharam 1440h, sawa na 19 Septemba 2018m safari itaanza saa nane mchana.
- - Wakazi wa mkoa wa Bagdad wakutane katika mji mtukufu wa Kadhimiyya barabara ya Imamu Swahibu Zamaan (a.f), safari itaanza saa kumi na mbili asubuhi ya siku ya Alkhamisi 10 Muharam 1440h sawa na 20 Septemba 2018m.
Tambua kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa magari ya kubeba mazuwaru bure pamoja na sehem za kupumzika na chakula.
Na itaandaliwa ratiba kamili ya kuomboleza itakayo jumuisha mambo yafuatayo:
Kwanza: usomaji wa Qur’an ikiwa kama sehemu ya kuwaenzi maswahaba wa Imamu Hussein (a.s) namna walivyo kesha katika usiku wa mwezi kumi Muharam.
Pili: majlis ya kusikiliza mawaidha na maelekezo mbalimbali pamoja na uimbaji wa kaswida za kuomboleza na kupiga matam.
Tatu: kusoma maktal (kuuwawa) kwa Hussei Alfajiri ya siku ya kumi.