Huseiniyya kadhaa za mawakili wa mkoa wa Karbala zimeshiriki katika maukibu moja ya kuomboleza katika maombolezo haya ya Ashura, yaliyo umiza kizazi kitukufu cha Mtume na umma wa kiislamu kwa kuuwawa Imamu Hussein (a.s), mamia ya mawakili wamefanya matembezi ya kuomboleza yaliyo anzia katika barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakaingia hadi katika uwanja wa haram yake tukufu, kisha wakatembea hadi katika malalo ya Imamu Hussein (a.s) wakipitia eneo la katikati ya haram mbili tukufu, matembezi yao yakaishia katika uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) na wakafanya majlis ya kuomboleza na kupiga matam.
Wakati wa matembezi yao walikua wanaimba kaswida zilizo jaa maneno ya huzuni zinazo amsha hisia za majonzi ya msiba huu, wakisisitiza kua matembezi haya ambayo hufanywa kila mwaka, wanayafanya kwa ajili ya kuenzi misingi na malengo ya muhanga wa Twafu, ambao ni taa linalo angazia walimwengu wote na kuwafundisha mambo mengi, ni muhimu kwa sasa misingi hiyo ifundishwe katika selebasi za malezi.