Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.
Na wabashirie wanao subiri. Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake yeye hakika tutarejea.
Amesema kweli Mwenyezi Mungu mtukufu.
Kwa majonzi makubwa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa pole kwa kifo cha Ustadh Allamah Sayyid Muhammad Ali Halo (Mwenyezi Mungu amuweke mahala pema peponi) aliye fariki siku ya Juma Nne (8 Muharam 1440h) sawa na (18 Septemba 2018m) baada ya kusumbuliwa na maradhi.
Umri wake wote ameutumia katika kuhudumia Dini ya kiislamu na sheria ya mbora wa Mitume (s.a.w.w), tunamuombea makazi mema peponi karibu na Mtume (s.a.w.w) na Maimamu watakasifu (a.s) na wanachuoni wema, tunamuomba Mwenyezi Munu ampe rehma nyingi zaidi katika siku hizi za Ashura na aipe familia yake subira pamoja na wapenzi wake hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.