Kutoka katika mji mkuu wa maadhimisho ya Husseiniyya: kituo cha uzalishaji na matangazo ya moja kwa moja Alkafeel kimefanya kila kiwezalo kumfanya mfuatiliaji wa matangazo awe kama yupo ndani ya matukio ya Ashura…

Maoni katika picha
Wataalamu wanao fanya kazi katika kituo cha uzalishaji na matangazo ya moja kwa moja chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya kila wawezalo kuhakikisha wanarusha pisha halisi za maombolezo ya Ashura kutoka makao makuu yake ambayo ni mji mtukufu wa Karbala, na kuzifikisha kila kona ya Dunia, kwa ajili ya kufanikisha hilo kitengo hiki kinafanya kazi kwa ufundi na uweledi wa hali ya juu.

Mkuu wa kituo Ustadh Bashiru Taajir ametuambia mpango maalumu wa kurusha matukio ya Ashura, amesema kua: “Kituo kilianza kujiandaa kurusha picha halisi za matukio ya Ashura, hakika wataalamu wetu wana uwezo na uzowefu mkubwa unao wawezesha kufanya jambo lolote la kiufundi, kutokana na utalamu wao wanaweza kupiga picha bora na kuzirusha katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iraq, wameweza kufanya hivyo kwa kutokea hapa Karbala tukufu mahala wanapo tamani wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait kuja kupaona”.

Akaongeza kua: “Kazi yetu inafanyika kipindi chote cha mwaka lakini wakati wa ziara na matukio ya Dini likiwepo tukio la Ashura hali hua tofauti, hua tunaandaa utaratibu unao tuwezesha kurusha matukio yote ya maombolezo katika Ataba mbili tukufu na katika eneo la katikati ya Ataba mbili, kazi ya kurusha matangazo haya inaendelea saa ishirini na nne katika vituo vya luninga (tv), kupitia masafa maalumu yenye ubora wa hali ya juu kwa kutumia anuani zifuatazo:

SAT:INTELSAT 902@62°E
DL:11457.5V
SR:3000
DVBS2
8PSK
FEC 2/3
HD/MPEG-4
akafafanua kua: Unaweza kufuatilia matangazo au kupakua kwa kutumia youtube: https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw
au unaweza kuangalia matangazo ya moja kwa moja kupitia facebook: https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: