Kuunganisha vizazi kifikwa katika jambo la Imamu Hussein (a.s): Ripoti ya picha za ushiriki wa watoto katika mawaakibu za kuomboleza…

Maoni katika picha
Ushiriki katika kuhuisha maadhimisho ya Husseiniyya kwa kuomboleza au kutoa huduma au kuhudhuria katika majaalisi hakuna umri maalumu, kila mtu anavutiwa kimaumbile kuhudhuria, kwa sababu Hussein (a.s) alijitolea kila kitu na matukio ya Karbala yanadhihirisha jambo hilo, utawaona watoto wakiwa na hamasa kubwa ya kushirikiana na wazazi wao katika kuhuisha maombolezo haya, na wao ipo siku watabeba urithi huo kama walivyo beba baba zao na babu zao mpaka ukawafikia, utawaona mara wanapiga matam mara wanalia wanawaiga wakubwa namna wanavyo fanya.

Huu ni utamaduni maalumu unao lenga kuunganisha kizazi na kizazi kifikra kuhusu Imamu Hussein (a.s), ukizingatia kuwa vita ya Karbala ilihusisha watoto wadogo kama wao kutoka katika familia ya Imamu Hussein (a.s) na maswahaba wake.

Wazazi wa watoto wanaoshiriki katika maombolezo haya wamesema kua ushiriki wao ni ujumbe wa wazi wa kurithishana utamaduni huu kizazi baada ya kizazi, kama tulivyo rithi sisi kutoka kwa wazazi wetu yatupasa kuwarithisha watoto wetu na wajukuu wetu, njia nzuri ya kurithishana ni kuwashirikisha katika maadhimisho mbalimbali ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: