Mwendelezo wa uhuishaji wa maombolezo ya Ashura: maukibu ya wanafuzi wa Dini katika mkoa wa Karbala…

Maoni katika picha
Kutokana na ukweli wa beti za kaswida ya Sharifu Ridhwa (q.s) isemayo: (Karbala utaendelea kua karban wa balaa ** kwa yale waliyo yapata kwako Aalu Mustwafa), jioni ya siku ya tisa Muharam, maukibu ya wanafunzi wa Dini wa mkoa wa Karbala imefanya matembezi ya kuomboleza na kumpa pole Swahibu Asri wa Zamaan (a.f) kwa kifo cha babu yake Abu Abdillahi Hussein (a.s), maukibu iliyokua na wanachuoni wengi pamoja na wanafunzi wa hauza za Dini kutoka mkoa wa Karbala.

Matembezi hayo yalianzia mbele ya (Mukhayyamu Husseiniyyi) wakitanguliwa na waandishi wa habari pamoja na mabango na kuelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakipitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kaswida na mashairi yaliyo kuwa yakisomwa yalipata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, matembezi hayo yaliishia katika uwanja wa haram ya Abu Abdillahi Hussein (a.s) na kufanya majlis ya kuomboleza ambayo ilipambwa na mashairi yaliyo jaa huzuni, majlisi ilijaa vilio, waumini walitokwa machozi wakati walipo kua wakisikia mambo ya kuumiza na ya kinyama yaliyo fanyiwa watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Kumbuka kua maukibu ya wanafundi wa hauza za Dini ni miongoni mwa maukibu za Ashura ambazo hufanya matembezi kila mwaka katika usiku wa kumi Muharam.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: