Kumuenzi Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba wake: Maahadi ya Qur’an tukufu yaendesha kisomo cha Qur’an cha Ashura…

Maoni katika picha
Kumuenzi Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba wake ambao walikesha wakisikika kama mlio wa nyuki kwa kuswali na kufanya ibada sambamba na kusoma Qur’an tukufu, Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya imeendesha zowezi la usomaji wa Qur’an tukufu ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Muharam kumi (1440h) sawa na (20 Septemba 2018m).

Usomaji huo umehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru ambao wamesoma majuzuu ya Qur’an tukufu yaliyo gawiwa kwao, jambo hili linaonyesha utukufu wa ibada ambazo Imamu Hussein (a.s) alikubali kujitolea muhanga kwa ajili yake.

Tunapenda kusema kua Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya hufanya harakati mbalimbali pamoja na mahafali za usomaji wa Qur’an katika matukio tofauti kwa lengo la kueneza uwelewa wa Qur’an katika jamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: