Miongoni mwa ratiba ya utowaji wa huduma kwa mazuwaru wa Ashura iliyo andaliwa na kitengo cha mgahawa (mudhifu) cha Atabatu Abbasiyya, ni kuandaa maelfu ya chakula na kukigawa kwa mazuwaru kupitia vituo mbalimbali vya ugawaji wa chakula, chakula hicho hawakupewa mazuwaru peke yao, bali walipewa vilevile watumishi na wafanya kazi wa kujitolea pamoja na wageni wa Ataba tukufu.
Rais wa kitengo cha mgahawa bwana Kaadhim Ibaadah ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika maandalizi ya ziara hii yalianza mapema, tuliweka stoo vyakula vingi vya aina tofauti, pamoja na maji na juisi na vitu vingine vinavyo hitajika katika chakula kwenye kipindi hiki cha ziara, mazuwaru walipo anza kumiminika katika mji wa Karbala wapishi wakaanza kupika chakula kwa wingi na kukigawa kwa mazuwaru”.
Akaongeza kua: “Hakika ugawaji wa chakula katika kipindi hiki cha ziara hakuhusishi aina maalumu wala muda maalumu, ugawaji unafanyika muda wote kuanzia asubuhi hadi jioni, kupitia sehemu tatu ambazo ni: mgahawa wa Atabatu Abbasiyya tukufu, mgahawa wa watumishi na sehemu ya barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ugawaji wa chakula unamefanika kwa urahisi na kwa haraka sana”.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu ilikua imesha tangaza kukamilika kwa maandalizi yote ya kuwapokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika siku za Ashura, iliandaa mkakati shirikishi wa kuimarisha usalama na kutoa huduma na ikasema ni mkakati makini utakao saidia kupunguza usumbufu kwa mazuwaru na kuwawezesha kufanya ibada na ziara kwa amani na utulivu, na wamefanya kila wawezalo kuhakikisha jambo hilo.