Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya: Jumla ya mawakibu (15,000) za waombolezaji na watoaji wa huduma zimeshiriki katika ziara ya Ashura zikiwemo za kiarabu na kiajemi…

Maoni katika picha
Rais wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan amesema kua: “Idadi ya mawakibu zilizo shiriki katika ziara ya Ashura na zilizo sajiliwa rasmi na kitengo hicho mwaka huu wa 1440h zimefika (elfu 15), maukibu za waombolezaji na watoa huduma zikiwemo kutoka nchi za kiarabu na zisizo kua za kiarabu, hizo ndio maukibu zilizo fanya kazi zao ndani ya mipaka ya mkoa wa Karbala zikiwa zimesajiliwa rasmi bado kuna ambazo hufanya kila kuwa na usajili pamoja na wakazi wa Karbala ambao hutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru bila kusajiliwa na baadhi wa watu ambao huja kutoka mikowani na kutoa kuduma bila usajili”.

Akaongeza kua: “Mawakibu (2000) kati ya hizo ni za waombolezaji wa zanjiil na matam zinafanya shughuli za kuomboleza, na mawakibu (13,000) zinatoa huduma kwa mazuwaru, zinagawa chakula na vinywaji pamoja na sehemu za kulala na vitu vingine, miongoni mwa maukibu hizo kuna maukibu (20) kutoka Oman, Saudia, Kuwait, Iran, Marekani, India na Pakistan”.

Akafafanua kua: “Mawakibu nyingi zinakuwa na pande mbili, zinasehemu ya waombolezaji na watoa huduma na asilimia kubwa zitaendelea kutoa huduma hadi mwezi kumi na tatu Muharam wakiendeleza kazi walizo anza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu”.

Akabainisha kua: “Kitengo hiki kilifanya vikao kadhaa na wawakilishi wa mawaakibu kabla ya kipindi cha Ashura, kwa ajili ya kuhakikisha tunafanya vizuri na kwa namna inayo endana na utukufu wa eneo hili, na kuhakikisha tunaondoa vikwazo vyote katika utendaji wa shughuli hii tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: