Inatokea sasa hivi: kuanza maombolezo ya (towareji)…

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya leo mwezi kumi Muharam (1440h) sawa na (20 Septemba 2018m) yamefanyika matembezi ya kuomboleza ya towareji, matembezi hayo yameanzia katika eneo la Qantwaratu Salaam (umbali wa kilometa tano hadi kufika katika haram ya Imamu Hussein –a.s-) wakapitia barabara ya Jamhuriyya hadi katika malalo mawiti matukufu, malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, chini ya ulinzi mkali wa Ataba mbili tukufu.

Matembezi ya towareji ni maandamano yanayo hudhuriwa na mamilioni ya watu, hufanywa na makabila ya towareji (wilaya ya Hindiyya ambayo ipo katika mkoa wa Karbala na upo umbali wa kilometa 20), kuhuisha na kuitikia wito wa Imamu Hussein katika siku ya kumi ya Muharam ambayo Imamu Hussein (a.s) alisema: (hivi kuna msaidizi aje kutunusuru), Karbala ni moja ya sehemu wanapo kutana watu wengi zaidi duniani, ni jambo la pekee na la aina yake, haya ni maadhimisho ya kidini ya Husseiniyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: