Kwa picha: Hivi ndivyo matembezi ya Towareji yalivyo kuwa…

Maoni katika picha
Imekuwa kawaida kufanya matembezi ya kuomboleza ya Towareji kwa karne nyingi, maombolezo haya yalianzishwa na watu wa mji wa Towareji (uliopo umbali wa kilometa 20 kusini mashariki ya Karbala tukufu), wamekusanyika makundi ya waumini nje ya mji wa Karbala katika barabara ya (Towareji) karibu na eneo maarufu liitwalo (Qantwaratu Salaam).

Waombolezaji kutoka katika mji wa Towareji na Karbala tukufu pamoja na mikoa mingine ya Iraq hukusanyika hapo, hadi wafike zaidi ya watu milioni, pia wanapo ingia katika mji wa Karbala baadhi ya mazuwaru kutoka nchi mbalimbali huungana nao, sauti zao husikika zikiita (yaa Hussein… yaa Hussein) sauti hiyo hupasua anga na huonyesha ukubwa wa mapenzi kwa Ahlulbait (a.s), kama vile kundi hilo linakuja kumnusuru Imamu Hussein (a.s) lakini wamefika wakiwa wamechelewa, ikiwa tayali amesha uwawa, kwa hiyo wanajipiga vichwa na kusema: (yaa Hussein … yaa Hussein).

Safari yao huwanzia katika eneo hilo –Qantwaratu Salaam- wakipitia barabara ya Jamhuriyya, hutembea kilometa kadhaa kabla ya kufika katika malalo mawili matukufu ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), humalizia maombolezo yao katika malalo ya mhami wa familia na mnyweshaji wenye kiu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: