Mafuriko makubwa ya watu wamaliza maombolezo ya Husseiniyya makubwa zaidi Duniani na Atabatu Abbasiyya yatangaza kufanikisha mpango wake wa ulinzi na utowaji huduma katika ziara ya Ashura…

Maoni katika picha
Mafuriko makubwa ya watu wamemaliza maombolezo ya Husseiniyya makubwa zaidi Duniani nayo ni maombolezo ya Towareji yanayo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ambayo yalianza baada ya swala ya Adhuhuri ya siku ya (10 Muharam 1440h sawa na (20 Septemba 2018m) na yakaendelea kwa zaidi ya saa tatu, wameshiriki makundi kwa makundi ya wafuasi na wapenzi wa Ahlulbait (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq chini ya ulinzi mkali na huduma bora kutoka kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na makundi ya watu wanaojitolea, wamepelekea utekelezaji wa maombolezo kuwa mwepesi na ukamilike bila tukio lolote la uvunjifu wa amani.

Kwa upande mwingine Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa mpango wake wa ulinzi na utowaji wa huduma walio andaa kwa ajili ya ziara ya Ashura, ambao umetekelezwa katika siku zote kumi na kuleta mafanikio makubwa katika mpangilio na utowaji wa huduma kwenye maombolezo ya Towareji na mengine yaliyo fanyika kabla yake, ambapo waombolezaji waliongezeka sana tangu siku ya saba ya mwezi wa Muharam, mafanikio haya ni muendelezo wa mafanikio ya ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu na sehemu ya kujiandaa kuelekea katika ziara ya Arubaini, mafanikio haya yametokana na kazi kubwa iliyo fanywa na vitengo tulivyo shirikiana navyo na kufanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kufanikisha ibada ya ziara kwa mpangilio mzuri na huduma bora.

Baada ya kukamilika ziara hii tutaingia katika hatua ya pili ya utendaji nayo ni kusafisha ndani na nje ya uwanja wa haram tukufu pamoja na njia zoto zinazo elekea katika Ataba tukufu pamoja na kuondoa mchanga milangoni na sehemu zingine iliyo patikana kutokana na ujio wa waombolezaji.

Idadi ya mawaakibu za waombolezaji pamoja na za kutoa huduma ilifika (15,000), zilizo sajiliwa ramsi na kufanya kazi ndani ya mipaka ya mkoa mtukufu wa Karbala, na idadi ya waandishi wa habari walio fanya kazi ndani ya Atabatu Abbasiyya pekeyake ilifika (250) kutoka katika luninga, redio na magazeti, baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kutoka kwa viongozi wa serikali ya mkoa wa Karbala kuwa: “Idadi ya mazuwaru ilikua zaidi ya milioni tatu miongoni mwao (elfu 34) kutoka nje ya Iraq”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: