Kwa ambaye aliniahidi kubaki kisha akaondoka.

Maoni katika picha
Kwa ambaye aliniahidi kubaki kisha akaondoka, imekua miaka ya matatizo magumu, huu hapa usiku wa mwezi kumi na moja Muharam umeingia na kutanda giza lake, umemaliza siku itishayo isiyo kuwa na mfano katika historia, miili yenu mitakatifu imesambaa juu ya udongo ikiwa imekatwa katwa, huu hapa mwili wa walii wa Mwenyezi Mungu Abu Abdillahi Hussein, karibu yake kuna miili ya watoto wake watukufu Ali Akbaru na Abdullahi aliye kua bado ananyonya, na ndugu zake Abbasi, Jafari, Othumani na Abdullahi ambao ni watoto wa Ummul Banina, pia kuna Kassim mtoto wa ndugu yake Imamu Hassan Almujtaba na watoto wa ammi zake miongoni mwa wanafamilia wa Abu Twalib, na kundi la maswahaba wake watukufu.

Amani iwe juu yako ewe bwana wa maji, umefika wakati wa muondoka, msafara wa mateka ikaanza kuelekea sham katika msafara ngumu mno, wakiwa pamoja na vichwa vya wapenzi wao vimetungikwa juu ya mikuki..

Karbala mwaka 1440h, mawakibu za waombolezaji wa Ashura zinaendelea kumiminika kutokana na mila za watu wa Karbala, jioni ya Juma Nne (10 Muharam 1440h) –ni usiku wa wahsha kwa Imamu Hussein “a.s”-) kuja kumpa pole bibi Zainabu na Imamu Sajjaad (a.s) kufuatia mambo yaliyo watokea katika siku hizo, na kukumbushana hali ya mayatima na wanawake wa familia ya Mtume (a.s) na kusoma maombolezo katika usiku wa kumi na moja, yakifungamana na maigizo ya yale yaliyo tokea kwa watu wa nyumba ya Imamu Hussein (a.s) wakiwemo watoto na wanawake, na waliyo endelea kufanyiwa.

Wakati wa matembezi ya mawakibu zilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, jambo lililo dhihirisha majonzi na huzuni kubwa waliyo kuwa nayo watu wa nyumba ya Mtume (a.s). Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimewasha taa nyekundu ndani ya haram zao tukufu kama ishara ya kuomboleza, pia mazuwaru wengi wamewasha mishumaa ndani ya Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: