Zaidi ya vyombo vya habari (250) vimeshiriki kutangaza matukio ya Ashura.. na uwepo wa pekee wa wataalamu wa habari wa Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Yasiri amesema kua: “Idadi ya vyombo vya habari vilivyo shiriki kutangaza matukio ya ziara ya Ashura mwaka huu ilikua zaidi ya (250), vikijumuisha vituo vya luninga (tv), redio, magazei, majarida pamoja na mitandao ya kielektronik kutoka ndani na nje ya Iraq, asilimia kubwa ya vyombo hivyo vilianza kurusha matangazo yao tangu siku ya kwanza ya Muharam, wameweza kufikisha picha na sauti za waombolezaji wa Imamu Hussein kila sehemu ya Dunia”.

Akabainisha kua: “Hakika kitengo hiki kiliwawekea mazingira rafiki yaliyo warahisishia utendaji wao, kila mwanahabari alipewa kitambulisho maalumu kilicho muwezesha kwenda kwa urahisi sehemu yeyote katika Ataba mbili na katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, vyombo vya habari vilivyo shiriki mwaka huu vimezidi idadi ya vyombo vilivyo shiriki mwaka jana, hii inamaanisha kuongezeka kwa kiwango cha utangazaji wa maombolezo ya Husseiniyya”.

Akaendelea kusema kua: “Pamoja na wingi wa vyombo vya habari, vyombo vya habari ambavyo vipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu vimeonyesha upekee katika sekta zake zote, sekta ya habari za kusomeka, kusikika na kuangalika, kituo cha uzalishaji na upigaji picha Alkafeel kimeonyesha mafanikio makubwa kwa kutengeneza masafa maalumu ya bure kwa ajili ya kurusha matukio ya ziara ya Ashura kwa ubora mkubwa unao wezesha chombo chochote cha habari kupata matangazo hayo kupitia masafa hiyo, kuanzia siku ya kwanza ya mwezi wa Muharam na itaendelea hadi mwezi kumi na tatu Muharam, hali kadhalika idhaa ya Alkafeel kupitia vipindi vyake vya redio, kuhusu mitandao ya kielektronik, mtandao wa kimataifa Alkafeel ulikua chanzo kikubwa cha habari za kielektronik kupitia ripoti zake za habari na sauti.

Kumbuka kuwa matangazo ya habari yalihusisha:

  • 1- Matukio ya uombolezaji yaliyo fanywa na mawakibu za kuomboleza na za kutoa huduma.
  • 2- Huduma zinazo tolewa na Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya.
  • 3- Huduma zinazo tolewa na mawakibu kwa mazuwaru.
  • 4- Mambo yote yanayo tokea katika mji wa maombolezo Karbala tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: