Vituo vya Ashura: Mwezi kumi na mbili Muharam kuwasili kwa mateka wa Imamu Hussein (a.s) katika mji wa Kufa…

Maoni katika picha
Mwezi kumi na moja Muharam watu wa nyumba ya Mtume (a.s) waliotekwa walianza safari ya jangwani, baada ya unyama mkubwa walio fanyiwa na kuwa na usiku mgumu walio lala karibu na miili ya ndugu zao walio uwawa kishahidi, msafara huo wa mateka uliwasiri katika mji wa Kufa siku ya kumi na mbili Muharam mwaka wa (61h), watu wa Kufa wakafadhaika, wakatoka barabarani baadhi yao wakiwa hawawajui mateka hao ni wakina nani na wengine wanawajua na huku wanalia na kujipiga kwa uchungu.

Baada ya mateka hao kuwasili Kufa walipelekwa katika kasri la mtawala, pamoja na kundi la watu wa Kufa wakiwa wanalia kwa uchungu kutokana na mambo waliyo fanyiwa watu wa nyumba tukufu ya Mtume (s.a.w.w) na Imamu wa waislamu Hussein (a.s), na sasa familia yake wameletwa wakiwa ni mateka, na kichwa cha mjukuu wa Mtume kinazungushwa katika mji wa Kuja kikiwa juu ya mkuki mrefu, na wao ndio walimwita aje kuwa kiongozi wao atakaye waelekeza katika njia ya uongofu.

Wakati wanatembea bibi Zainabu (a.s) aliwaangalia watu waliofurika kuwashangaa, kwa hasira ya kuuliwa kwa kaka yake na udhalili wa kutekwa, aliwaangalia kwa hasira na akawahutubia kwa maneno makali nafasi haitoshi kuyaelezea hapa.

Kichwa cha Hussein (a.s) kikaingizwa katika qasri na kuwekwa mbele ya Ibun Ziyadi –laana ya Allah iwe juu yake- akaanza kukipiga piga na fimbo iliyokua mkononi mwake, akiwa na furaha kubwa, kisha wakaingizwa wanawake na watoto pamoja na Ali bun Hussein (a.s), Ibun Ziadi akaanza kumshutumu bibi Zainabu (a.s) kwa kusema: (Alhamdu lilahi ambaye amekufedhehesheni na kukuuweni na kadhibisha uzushi wenu), bibi Zainabu (a.s) akamrudishia kwa maneno ya kujiamini: (Alhamdu lilahi ambaye ametukirimu kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) na akatutwaharisha na uchafu, hakika hufedhehesha mafasiq na hudhihirisha uongo wa waovu na hao sio sisi).

Ibun Ziyadi akasema: Umeonaje Mwenyezi Mungu alivyo wafanya watu wa nyumbani kwako? Bibi Zainabu (a.s) akasema: (Mwenyezi Mungu amewaandikia kifo wamepigana hadi wakauwawa kishahidi, na Mwenyezi Mungu atawakutanisha na wewe na mtahojiana mbele yake).

Ukaja muda wa Imamu Sajjaad (a.s) akasimama mbele ya Ibun Zayadi, akaulizwa: nani wewe? Akamjibu: (Mimi ni Ali mtoto wa Hussein). Akasema: Mwenyezi Mungu hajamuua Ali bun Hussein? Akamjibu: (Nilikua na ndugu yangu anaitwa Ali bun Hussein ameuliwa na watu). Ibun Ziyadi akasema: Bali kauliwa na Mwenyezi Mungu. Akamjibu: (Mwenyezi Mungu huchukua nafsi wakati wa umauti wake), Ibun Ziyadi akakasirika kutokana na majibu hayo, akamwita Jalawizah: akasema mkate chichwa chake. Shangazi yake Zainabu (a.s) akamkumbatia na akasema kwa sauti ya ukali: (Ewe Ibun Ziyadi inatosha kumwaga damu zetu, wallahi sitamuachia kama unamuuwa niuwe pamoja naye) Ibun Ziyadi akaacha kumuuwa.

Chuki ya Ibun Ziyadi na ugumu wa roho yake pamona na matendo ya kinyama viliendelea, siku ya pili kichwa cha Imamu Hussein kikazungushwa katika mitaa ya mji wa Kufa, kuwatisha watu wa Kufa na kumuonya yeyote atakaye fikiria kufanya upinzani.

Fahamu kua harakati ya Imamu Hussein (a.s) ilipitia hatua nyingi, ikiwa ni pamoja na ile ya karibu na kifo chake (a.s) na yaliyo endelea baada ya kifo chake, miongoni mwa hatua hizo ni kuwasili kwa mateka wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Kufa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: