Zaidi ya maukibu (116) za makabila na koo za Iraq yameshiriki katika kumbukumbu ya kuzikwa miili mitakasifu…

Maoni katika picha
Katika kuhuisha maombolezo ya Ashura ya Imamu Hussein (a.s) kuna vitendo na ada tofauti, zote ninalenga kuomboleza mauwaji ya Twafu na matukio yaliyo fuatia, ikiwemo yaliyo fanyika mwezi kumi na tatu Muharam ya kuzikwa mwili wa Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) pamoja na maswahaba wake baada ya kukaa siku tatu juu ya jangwa la Karbala.

Watu wa Karbala wamezowea kukamilisha maombolezo ambayo huanza siku ya kwanza ya Muharam kwa kufanya kumbukumbu ya tukio hili, ambapo hutoka makabila na koo za mkoa huu pamoja na wanaokuja kutoka mikoa mingine ya Iraq, wakiongozwa na kabila la bini Asadi lililo pata utukufu mwaka (61h) wa kumsaidia Imamu Sajjaad (a.s) kuzika miili ya mashahidi wa Twafu.

Waombolezaji husimama kwa vikundi, kila kikundi huwakilisha kabila linalo shiriki katika maombolezo hayo ambayo hufanywa kila mwaka, wakitanguliwa na pendera za Husseiniyya na viongozi wa kabila husika, huku wakipiga vifua vyao na wakiwa wamebeba vitu wanavyo igiza kama miili ya mashahidi wa Twafu pamoja na baadhi ya vifaa vya zamani vilivyo kua vikitumika katika kuchimbia kaburi na mazishi, makabila yote hutanguliwa na kabila la mama wa msiba (kabila la bani Asadi).

Waombolezaji wa kike hawakubaki nyuma, wameshiriki kwa wingi wakiwa wamepaka tepe nyuso zao, kama ishara ya msiba na kumpa pole bibi Zainabu (a.s) kutokana na msiba huu mkubwa, pamoja na kukariri mimbo inayo onyesha kushikamana kwao na mafundisha ya Muhammadiyya na kuendeleza mwenendo wa Husseiniyya ulio anzishwa na bwana wa mashahidi Imamu Hussein (a.s) kwa kumwaga damu yake takatifu hapa Karbala.

Maukibu zilianza matembezi yao baada ya swala za Dhuhurain jirani na malalo ya bwana wa uzuri (Sayyd Juud) mashariki ya mji wa Karbala, (ambaye ni mmoja wa viongozi wetu na inasemekana ndio mwanzilishi wa aina hii ya uombolezaji), wakaelekea katika barabara inayo zunguka mji wa zamani, kishwa wakatembea hadi katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) wakaenda hadi katika malalo yake tukufu, halafu wakatoka na kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili na wakaishia katika malalo ya mbeba bendera Abulfadhil Abbasi (a.s).

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Miongoni mwa majukumu yetu kama kitengo tumeandaa mazingira ya kuwapokea waombolezaji kwa kushirikiana na vitengo vingine vya Ataba tukufu, idadi ya maukibu zinazo shiriki katika maombolezo haya ni zaidi ya (116) kutoka ndani na nje ya Karbala, baadhi yao wameomboleza asubuhi ya leo lakini wengi wao wameomboleza kama wanavyo fanya kila mwaka, mawakibu zimetembea kwa amani na utulivu chini ya utaratibu maalumu ulio wekwa kwa ajili ya kuepuka msongamano, mawakibu ziliendelea kumiminika ndani ya muda wa saa nne takriban, mawakibu za kutoa huduma ziliwahudumia kwa namna walivyo weza”.

Kwa maombolezo haya machungu ndio yanafunga pazia la kuomboleza mauwaji ya Twafu, aliyo fanyiwa Imamu Hussein (a.s) na kumwaga damu yake tukufu ambayo itaendelea kuwa taa milele na milele kwa kila mtu huru Duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: