Maukibu (Kandili za mbinguni) yahuisha maombolezo ya mwezi kumi na tatu Muharam…

Maoni katika picha
Uhuishaji wa kumbukumbu ya siku tatu baada ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wake wema katika vita ya Twafu, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia wafanyakazi wake wamefanya maukibu (maombolezo) ambayo hufanywa kila mwaka kwa jina la (Kandili za mbinguni), watumishi wa Ataba tukufu wamesimama pamoja na baadhi ya watoto wakiwa wamevaa nguo nyeupe na wapenyanyua mabango yaliyo andikwa majina ya mashahidi wa vita ya Twafu pamoja na mauwa.

Matembezi hayo; yalitanguliwa na watu walio beba bendera na misahafu, yalianzia katika uwanja wa haram tukufu ya Abbasi kwenye mlango wa Alqami (Furat) baada ya swala ya Isha na kuelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s) wakipitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, wakiwa wamejaa huzuni kutokana na yaliyo fanyika katika vita ya Twafu yanayo endelea kuumiza roho za wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), matembezi yakaishia katika uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlis iliyopata mwitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru watukufu, yalisomwa mashairi ya Husseiniyya yanayo huzunisha ,watu wakalia na kupiga matam kama sehemu ya kuhuisha maadhimisho ya Mwenyezi Mungu.

Kumbuka kua mji wa Karbala Juma Pili ya leo baada ya swala ya Dhuhurain umeshuhudia uombolezaji wa mazishi ya Imamu Hussein (a.s) ambao uliongozwa na maukibu ya kabila la bani Asadi kwa kushirikiana na makabila mengine ya Karbala na maeneo yanayo izunguka, walio zikwa siku ya tatu baada ya kuuwawa kwao kishahidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: