Jopo la wataalamu katika ujumbe wa mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu: Maji safi yatafika Abu Khaswiib na Baradhiiyya ndani ya siku chache…

Maoni katika picha
Mkuu wa ofisi ya mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji wa Basra ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Jopo la wataalamu walio pewa jukumu na mwakilishi wa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ahmad Swafi, ambaye na yeye alipewa jukumu na Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani la kuja kusaidia utatuzi wa tatizo la maji safi ya kunywa katika mji wa Basra, wanaendelea na kazi zao zilizo anza (2 Septemba 2018m), wanaendelea kuondoa vizuwizi vya maji vilivyopo katika kituo cha maji na katika mabomba yanayo peleka maji katika mji wa Abu Khaswiib, moja ya miji ya mkoa huo, kazi hiyo imesababisha kukatika maji kwa muda katika baadhi ya maeneo na yatarudi moja kwa moja baada ya kumaliza kuondoa vizuwizi vyote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Ustadh Jawadi Hasanawi akasisitiza kua: “Kazi ya kufunga mashine mpya za kusukuma maji inaendelea katika matawi ya mji wa Baradhiiyya Basra kwa ajili ya kuwafikishia maji safi”.

Akasisitiza kua “Maji safi yatafika katika miji yote miwili ndani ya siku chache zijazo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Kumbuka kua Marjaa Dini mkuu alimuagiza mwakilishi wake Sayyid Ahmadi Swafi mwanzoni mwa mwezi wa Septemba kwenda kusaidia kutatua tatizo la maji safi ya kunywa katika mkoa wa Basra, na alitekeleza jukumu ndani ya siku 15 akawa kapiga hatua kubwa, akaahidi kua jopo la wataalamu alio kwenda nao wataendelea na kazi kwa muda wa mwaka mzima, kwa ajili ya kukamilisha na kusimamia kazi yao, ikiwa ni pamoja na kuondoa vizuwizi katika mabomba yanayo safirisha maji, na kufunga mashine za kusukuma maji katika matawi ya vituo vya maji yanayo ungana na kituo cha Albid’ah, pamboja na kutengeneza mfumo wa ulinzi na kuweka baadhi ya mikakati itakayo dumisha uwopo wa maji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: