Imamu Zainul-Aabidina (a.s) aukumbatia mwili wa ammi yake Abbasi na kubusu shingo lake takatifu…

Maoni katika picha
Baada ya Imamu Zainul Aabidina (a.s) kuzika mwili wa baba yake na watu wa nyumbani kwake pamoja na maswahaba zake, aliwaangalia bani Asadi alio kua nao katika mazishi, akawaambia: (Angalieni je kuna yeyote aliye baki bila kuzikwa?).

Wakasema: Ndio, kule karibu na mto Alqami kuna mwili bado haujazikwa, umekatwa katwa vipande vipande, kila tukiunyanyua upande mmoja upande mwingine unaanguka chini.

Akalia (a.s) alipo sikia hivyo, akasema kwa huzuni kubwa: (Enyi bani Asadi mnajua ni mwili wa nani huo? Hakika ni mwili wa ammi yangu Abbasi –a.s-).

Kisha akaufuata, alipo fika na kuuona aliukumbatia na akaanza kuubusu katika shingo lake tukufu huku anasema: (Dunia baada yako ni chungu ewe mwezi wa bani Hashim, nakutakia amani ewe shahidi mwema na rehma za Mwenyezi Mungu na baraka zake).

Akachimba kaburi na akamzika peke yake kama alivyo mzika baba yake, akawaambia bani Asadi: (Hakika ninao wanao nisaidia).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: