Kumalizika maombolezo ya bani Asadi na kumbukumbu ya mazishi ya miili mitukufu kunazifanya mawakibu na vikundi vya kutoa huduka kukamilisha msimu wa kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya Ashura, zilizo anza tangu siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Muharam, ni mazowea ya watu wa Karbala kizazi baada ya kizazi kutoa huduma katika siku kama hizi, hii haizuwii watu wengine kutoa huduma lakini waanzilishi ni wao (watu wa Karbala), unapo karibia kuingia mwezi wa Muharam utawakuta wanajiandaa kwa ajili ya kutoa huduma.
Asilimia kubwa ya mawakibu kwa sasa zinakusanya vifaa vyao walivyo kua wakitolea huduma kama vile vyombo, vyungu madeli ya maji na vinginevyo na kuondoka, mawakibu hizo zilifanya kazi usiku na mchana sio kwa kuhudumia mazuwaru peke yao bali hata wakazi wa nyumba zinazo zunguka maukibu zao, wanatumia uwezo wao wote wa hali na mali na hushindana katika kutoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru na kuonyesha mapenzi makubwa kwa Imamu Hussein (a.s), huthibitisha kauli isemayo: (Watumishi wa Hussein –a.s- na mazuwaru wake ni fahari kwetu) kama walivyo kua mfano katika maombolezo ya Ashura pia wao ni mfano mwema katika ukarimu kwa ajili ya Hussein (a.s).
Wamemaliza msimu huku uhalisia wa mazingira yao unasema: Je! Tumetekeleza ewe Abu Abdillah? Laiti umri wote tungeutumia katika kuwatumikia mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s)…
Wamemaliza wakiwa wanategemea kuongeza huduma zaidi katika ziara ijayo…
Wamemaliza wakisema ewe bwana wa mashahidi: “Kila kilicho tolewa hakifikii ubora wa chembe ndogo ya mchanga ulio kanyagwa na mguu wako katika ardhi ya Karbala”.
Kumbuka kua idadi ya mawaakibu zilizo shiriki katika maombolezo ya Ashura ni (15,000) zikiwa maukibu (2,000) za kuomboleza na zanjiil pamoja na matam, na maukibu (13,000) za kutoa huduma kwa mazuwaru, kugawa chakula, vinywaji na kuandaa sehemu za kupumzika na kulala pamoja na mambo mengine.