Vituo vya Ashura: Bibi Zainabu (a.s) katika kikao cha maluuni Ibun Ziyadi…

Maoni katika picha
Katika siku kama hizi mwaka wa 61 hijiriyya maluuni Ibun Ziyadi alifanya mkutano mkubwa katika Kasri lake ambapo aliwaita viongozi wa jeshi lake na viongozi wa mji wa Kufa, akaamuru kiletewe kichwa cha Imamu Hussein pamoja na mateka, akiwa na lengo la kuwadhalilisha Ahlulbait (a.s), na kuonyesha chuki yake kwao pamoja na kuonyesha uwezo wake na kutia hofu katika nyoyo za watu.

Ibun Ziyadi akakaa katika kiti chake cha utawala akiwa amejaa furaha ya ushindi wake wa uovu, huku ameshika finbo na kuchapa chapa kichwa cha Hussein (a.s) pamoja na kukichoma choma mdomoni.

Shekh Mufiid katika kitabu cha (Irshadi) anasema kua: (Familia ya Hussein ikaingizwa kwa Ibun Ziyadi, bibi Zainabu dada yake Hussein alikua miongoni mwa walio ingizwa akiwa amevaa ngua dhalili sana, aliingia na akaenda kukaa pembozobi mwa Kasri, Ibun Ziyadi akasema: nani yule aliye kaa pembeni akiwa na wanawake?! Zainabu hakumjibu, akauliza mara ya pili na ya tatu. Baadhi ya watu wake wakamwambia; Huyu ni Zainabu mtoto wa Fatuma mtoto wa Mtume wa Mwenyezi mungu. Ibun Ziyadi akamgeukia na kumwambia: Alhamdu Lillaahi ambaye kakufedhehesheni na kakuuweni na kakadhibisha uzushi wenu, : bibi Zainabu (a.s) akasema: Alhamdu lilahi ambaye ametukirimu kwa Mtume wake Muhammad (s.a.w.w) na akatutwaharisha na uchafu, hakika hufedhehesha mafasiq na hudhihirisha uongo wa waovu na hao sio sisi.

Ibun Ziyadi akasema: Umeonaje Mwenyezi Mungu alivyo wafanya watu wa nyumbani kwako? Bibi Zainabu (a.s) akasema: Sijaona jambo lolote kwao ispokua ni zuri, Mwenyezi Mungu amewaandikia kifo wamepigana hadi wakauwawa kishahidi, na Mwenyezi Mungu atawakutanisha na wewe na mtahojiana mbele yake tutaona nani mwenye faraja siku hiro, mama yako amekukosa ewe mtoto wa Marjana.

Ibun Ziyadi akachukia na akahamaki kwa maneno hayo, Amru bun Harithi akamwambia: Ewe kiongozi, hakika huyu ni mwanamke na mwanamke haadhibiwi kwa maneno yake. Ibun Ziyadi akasema: Mwenyezi Mungu amesha ponya roho yangu kwa kifo cha muovu wako Hussein na kundi la waasi katika Ahlulbait wake.

Zainabu akalia na akasema: Naapa kwa umri wangu hakika umeuwa burudisho la macho yangu, na umekata sehemu ya mwili wangu, na umeng’oa shina langu, kama hiyo nduio ponyo yako kwa hakika umepona.

Ibun Ziyadi akasema: Huyu ni mfasaha, naapa kwa umri wangu hakika baba yake alikuwa mfasaha na mshairi. Kisha akamgeukia Ali bun Hussein akamuuliza: nani wewe? Akamjibu (a.s): Mimi ni Ali bun Hussein. Ibun Ziyadi akasema: Mwenyezi Mungu si amesha muuwa Ali bun Hussein? Akasema (a.s) Nilikua na ndugu yangu anayeitwa Ali bun Hussein kauliwa na watu. Ibun ziyadi akasema: Bali kauliwa na Mwenyezi Mungu. Akamjibu (a.s): (Mwenyezi Mungu huchukua nafsi wakati wa umauti wake), Ibun Ziyadi akakasirika na akasema umekuwa jeuri katika kunijibu, akaagiza waende kukate chichwa chake. Shangazi yake Zainabu (a.s) akamkumbatia na akasema kwa sauti ya ukali: (Ewe Ibun Ziyadi inatosha kumwaga damu zetu, wallahi sitamuachia kama unamuuwa niuwe pamoja naye) Ibun Ziyadi akamwangalia bibi Zainabu na akamwangalia Ali akasema: Ajabu sana undugu! Wallahi mimi nafikiri nilimuuwa pamoja naye, muacheni mimi taangalia ana nini.

Kisha Ibun Ziyadi akaamrisha Ali bun Hussein na watu wake wapelekwe kwenye nyumba iliyo kua pembeni ya msikiti mkubwa, Zainabu bint Ali akasema: Hataingia hapa muarabu ispokua mama wa mtoto mmilikiwa, hakika wao wametekwa na sisi tumetekwa.

Katika mazungumzo hayo mafupi alibainisha kheri na shari, utukufu na udhalili, utakasifu na uchafu, walezi wa wahyi na upevu ya utume na muongo mtoto wa muongo! Ikawa wazi kaabisa pande zote mbili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: