Katika washiriki (150) wa mashindano wa kupiga picha yaliyo fanyika nchini Bahrain: Atabatu Abbasiyya tukufu yapata nafasi ya pili…

Maoni katika picha
Watumishi wa Abbasi (a.s) bado wanang’aa katika mahafali za kimataifa na kitaifa, wataendelea kung’aa kwa sababu wamepambika na baraka zake na ikhlasi yake pamoja na utendaji wake, miongoni mwa wapiga picha walio shiriki ni Saamir Husseini, ambaye ni mmoja wa wapiga picha wa kituo cha uzalishaji Alkafeel ambacho kipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Amepata nafasi ya pili kwenye mashindano yaliyo fanyika katika Husseiniyya ya bwana Ahmadi bun Khamisi nchini Baharain, yaliyo kuwa na washiriki (150) kutoka katika nchi tofauti za kiarabu, jumla ya picha zilizo shindanishwa zilikua (500) na zilichambuliwa na kamati ya watu walio bobea katika fani hiyo.

Husseini ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Nakabidhi ushindi huu kwa Maulana Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa sababu unatokana na baraka zake na ukarimu wake, napenda kubainisha kua; ushindi huu sio wa kwanza kwangu, nimesha shinda mara nyingi pamoja na kwamba mimi sio shabiki sana wa mashindano na wala sio kipao mbele changu, mimi naona kuitumikia taasisi ninayo fanya kazi ni bora zaidi kwangu kuliko kuitumikia nafsi yangu”.

Kumbuka kua vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake hushiriki mahafali nyingi za kimataifa na kitaifa, na wamefanikiwa kushinda katika mambo tofauti, kutokana na msaada wanaopata na ikhlasi katika kazi zao pamoja na kujituma kwao katika kuhakikisha pendera ya Atabatu Abbasiyya tukufu inakua juu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: