Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasoyya zitafanya majlis ya kuomboleza kifo cha Alamah Sayyid Muhammad Ali Halo siku ya Alkhamisi (17 Muharam 1440h) sawa na (27 Septemba 2018m) saa nane Adhuhuri, katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu.
Hii ni kutokana na kuonyesha thamani ya juhudi kubwa aliyo fanya katika sekta ya elimu, umri wake wote aliutumia katika kuhudumia Dini ya kiislamu na sheria za mbora wa Mitume (s.a.w.w).
Kumbuka kua marehemu Alamah Sayyid Muhammad Ali Halo alifariki siku ya Juma Nne (8 Muharam 1440h) sawa na (18 Septemba 2018m) baada ya kusumbuliwa na maradhi.