Tangazo la kuanza kazi ya idara ya utowaji wa misaada chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu…

Maoni katika picha
Asubuhi ya tarehe (17 Muharam 1440h) sawa na (27 Septemba 2018m) limefanyika kongamano la kwanza la idara ya utowaji wa misaada chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayo simamiwa na kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) katika mikoa (12), kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, lilifunguliwa kwa Qur’an kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Baada ya hapo ukafuata ujumbe wa kiongozi wa idara Shekh Abbasi Akashi ambaye alibainisha mazingira ya utekelezaji wa jukumu la kutoa misaada, na huduma gani zitakazo tolewa kwa vikosi vya askari pamoja na ushiriki wao katika kulinda amani kwenye misimu ya ziara.

Kisha ukafuata ujumbe wa kikosi wa wapiganaji cha Abbasi (a.s), ulio wasilishwa na mkuu wa kikosi hicho Shekh Maitham Zaidi ambaye amebainisha kua: “Mawakibu za kutoa misaada ni sehemu ya misaada ya mikakati –washirika wa ushindi- katika vita ya kuilinda ardhi heshima na maeneo matakatifu, iliyo tokana na mwitikio wa fatwa ya jihadi ya kujilinda iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Siatani”.

Akaongeza kua: “Tumekwisha bainisha na tunakumbusha tuliyo sema kutokana na umuhimu mkubwa wa kuanzishwa mradi huu, ukizingatia kua Mawakibu za kutoa misaada ya kimkakati ilikua na mchango mkubwa katika ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, na nyie mnafahamu msemo wa kiaskari usemao mwanajeshi hutembea kwa tumbo lake, jeshi lolote hapa Duniani linalo ingia vitani linahitaji mpangilio wa kiidara na kiutumishi pamoja na vifaa na siraha, Mawakibu za kutoa misaada ya kimkakati ziliziba pengo hilo”.

Akaendelea kusema kua: “Mimi naamini kua kama sio kuwepo kwa Mawakibu hizo ushindi huu usingepatikana kwa muda mfupi, mnafahamu wazi sio kila wizara ya serikali ilishiriki au kusaidia mapambano wakati wa vita, sisi tulipata tatizo la uwepo wetu, adui alikua hashambulii sehemu maalumu bali alipambana kuhakikisha tusiwepo, kwa hiyo tukapambania kuthibitisha uwepo wetu”.

Akaashiria kua: “Kwa masikitiko makubwa wizara zetu hazikuwepo katika uwanja wa vita jambo lililo sababisha raia wazibe pengo hilo, kwa kugawa chakula, dawa, maji hadi vifaa vya kiaskari, na wakati mwingine waliingia kupigana”.

Akasisitiza kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imelipa umuhimu swala la kuwakirimu mashujaa hawa, kutokana na juhudi zao, sio vizuri baada ya kumaliza vita tuwaambie: Mwenyezi Mungu atakulipeni na kuwaombea dua peke yake, kwa hiyo Ataba imeanzisha idara iitwayo; Idara ya misaada, kwa ajili ya kuendelea kusaidia vikundi vilivyo wasaidia askari”.

Akakamilisha kwa kusema: “Haifai mawakibu ziendelee kusaidia askari bila ukomo, ni wajibu kwa taasisi za serikali kutatua matatizo ya wapiganaji kwa kuwapatia maji ya kunywa na vyakula, jambo inalo pelekea baadhi ya viongozi wakusanye hela kutoka katika mishahara ya wapiganaji na kununua maji, na nyie mnafahamu mishahara ya Hashdi Sha’abi hailingani na mishahara ya askari wa vikosi vingine”.

Akamalizia kwa kusema: “Ziara ya arubani ijayo baada ya siku chache kwa mara ya kwanza Mawakibu ya misaada itashiriki, tumewaingiza katika ratiba ya kulinda amani kwenye ziara ya Arbainiyya, idadi ya watakao jitolea katika Mawakibu ya misaada ni elfu mbili, na zaidi ya watu elfu tatu watajitolea katika kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s)”.

Kongamano likafungwa kwa kipengele cha kujadiliana kuhusu vifaa vitakavyo tumika kutolea huduma katika siku chache zijazo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: