Watumishi wa Ataba mbili tukufu wanaomboleza siku ya saba baada ya kifo cha Imamu Hussein (a.s)…

Maoni katika picha
Kwa nyonyo zenye unyenyekevu na sauti za huzuni za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) leo Alkhamisi (17 Muharam 1440h) sawa na (27 Septemba 2018m) yamefanyika maombolezo ya pamoja ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ya kuomboleza siku ya saba baada ya kifo cha Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na maswahaba wake wema (a.s) na kumpa pole mjukuu wake Imamu Mahdi (a.f) kwa yaliyo jiri kwa babu yake, wamehuisha maombolezo katika mazingira ya liyo jaa huzuni na majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa wa kifo cha Imamu Hussein (a.s).

Matembezi ya maukibu hiyo ya kuomboleza yalianzia katika uwanja wa haram ya mbeba bendera na mnyweshaji wenye kiu Karbala Abulfadhil Abbasi (a.s), wakapitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu wakaenda hadi katika uwanja wa haram ya shahidi mtoto wa shahidi mwenye msiba mkubwa ambao haujawahi kutokea msiba unao fanana na msiba wake Imamu Hussein (a.s), na wakapokelewa na watumishi wa malalo yake tukufu.

Matembezi yalipambwa na kaswida pamoja na mashairi ya kuomboleza yanayo amsha hisia za huzuni kwa wapenzi na wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na wakamalizia katika uwanja wa haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanya majlis ya kuomboleza na kupiga matam.

Kumbuka kua Ataba tukufu za Karbala hufanya matembezi ya kuomboleza katika matukio ya kukumbuka vifo vya Ahlulbait (a.s) katika kipindi chote cha mwaka.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: