Miongoni mwa mikutano ya naibu rais wa umoja wa mataifa nchini Iraq, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi aelezea mambo muhimu kuhusu Iraq.

Sehemu ya kikao
Ugeni mkubwa maalumu ukiongozwa na naibu rais wa ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Iraq bibi Yunami Eliasi Walpole ulitembelea Atabatu Abbasiyya tukufu siku ya Juma Tano (16 Muharam 1440h) sawa na (26 Septemba 2018m).

Ugeni huo uliomba kukutana na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, katika kikao chao walijadiliana mambo mbalimbali na Mheshimiwa alijibu baadhi ya maswali yao kuhusu Iraq, ambapo walizungumzia mambo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Mtandao wa kimataifa Alkafeel ulikuwepo katika kikao hicho, na unakuletea baadhi ya mazungumzo hayo.

Bibi Yunami Eliasi Walpole alisema kua: Hii sio mara ya kwanza kutembelea Karbala, lakini ni mara ya kwanza kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu, napenda kukupongeza kwa kutatua matatizo ya Basra na mikoa ya kusini kwa njia ya amani, na wewe binafsi ulikua na nafasi muhimu, na kila mwislamu hasa wanao ishi katika mikoa ya kusini wanadeni kwako kutokana na kazi uliyo fanya.

Akamuuliza swali Mheshimiwa Sayyid Swafi: Napenda kusikia kutoka kwako kuhusu nafasi ya Marjaiyya tukiwa tunakaribia kipindi muhimu, kipindi cha kuunda serikali, unaona vipi nafasi ya Marjaiyya na nafasi yako binafsi katika kusaidia utulivu wa serikali mpya? Mna nia gani na matarajio gani kwa serikali ijayo na mnaushawishi gani kwa wananchi wa Iraq?

Mheshimiwa akamjibu: Sisi tunaheshimu nafasi ya umoja wa mataifa hapa Iraq pamoja na nchi zingine, mna athari kubwa katika mambo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, tunasumbuliwa na magenge ya watu wasio taka utulivu, kila nafasi ya umoja wa mataifa inavyo kua kubwa ndio hali ya utulivu inavyo kuwepo.

Akaongeza kua: Hatukatai kuwepo kwa matatizo mengi katika taifa letu, lakini nyenzo zote za maendeleo zipo, tatizo kubwa lililopo naweza kuligawa sehemu mbili. Kwanza: kukosekana uongozi bora wa serikali kwa ajili ya kutatua matatizo, pili: kuwepo kwa tatizo la ufisadi wa mali na kiuongozi, kimsingi hilo ndio tatizo lililo leta magaidi wa Daesh, hadi sasa serikali mpya haijaonyesha msimamo sahihi, kama mnavyo jua kua kuna mtazamo wa Marjaiyya nahisi jambo hili lipo wazi kwenu na kwa kila anaye fuatilia mambo ya Iraq, daima Marjaa Dini mkuu amekua akitetea maslahi ya raia wa Iraq, anatoa nasaha, ushauri na mwongozo, wala halengi kufanyia uwadui upande wowote utakao tekeleza majukumu yake ya msingi, lakini itakapo tokea chombo cha serikali kikaacha kutekeleza majikumu yake, bila shaka jambo hilo litasababisha matatizo kwa raia wa Iraq.

Marjaiyya anauhusiano mkubwa na wananchi, watu hurudi kwa Marjaiyya na kunufaika na mwongozo wake katika mambo binafsi na mambo ya kijamii, na Marjaiyya anayafanyia kazi matatizo ya raia na kutoa maelekezo ya kutatua shida za watu.

Akasisitiza kua: Kwa bahati mbaya katika viongozi wa serikali hakuna anaye sikiliza na kufuata maneno ya Marjaiyya, jambo hili limeleta matatizo makubwa mawili ambayo ni:

Tatizo la kwanza: Kuingia kwa Daesh na kuteka robo tatu ya Iraq, serikali ilishindwa na haikujua ifanye nini, jambo lililo pelekea Marjaiyya aingilie swala hilo kwa nguvu, na akatoa fatwa yake maarufu iliyo hami taifa la Iraq na mataifa mengine, ambayo iliitikiwa haraka na kuleta ushindi alhamdulilahi, wakati baadhi ya vyombo vya kimagharibi vilisema ukombozi wa taifa hili dhidi ya Daesh kwa uchache unahitaji miaka thelathini, lakini tukaweza kulikomboa ndani ya miaka mitatu kutokana na juhudi za wapiganaji.

Tatizo la pili: Tatizo la mji wa Basra ambalo kimsingi linafanana na matatizo yaliyopo katika mikoa mingine, wakati mwingine tatizo linafungamana na uhai wa watu moja kwa moja, tatizo hilo limetatuliwa kwa siku chache zisizo zidi siku (15) pia jopo la wataalamu wa ujumbe wa Marjaiyya bado lipo katika mji huo na wataendelea kubakia huko kwa muda wa mwaka mzima, kwa ajili ya kuzuia uharibifu, tayali maeneo mengi ya mji huo yamesha fikiwa na maji safi ya kunywa, na sehemu ambazo bado zitafikiwa hivi karibuni katika kipindi kisicho zidi siku (10), kuna maeneo ya njia za maji yalikuwa yamewekewa vizuwizi na watu wa mji huo, jambo lililo sababisha maji yasifike katika makazi ya watu, kwa hakika tatizo kubwa lililopo viongozi wengi wa serikali hawatumii mali za umma kwa umakini, na wala hawatumii mashirika bora na kuna kuingiliwa kazi na watu ambao hawana ujuzi nazo, inawezekana pia miongoni mwa matatizo makubwa ni pale mwanasiasa anapo kua mfanya biashara, lazima mambo yataenda kombo, haya ndiyo yanayo husu mji wa Basra.

Tuna mategemeo, ambayo yanaweza kutimia kama zikizingatiwa nasaha za Marjaiyya, Marjaiyya hataki kitu maalumu kwa ajili yake bali anataka mambo yatakayo wafaa raia, bila shaka serikali ni chombo cha kuhudumia raia, zinapo tajwa sifa maalumu za watu wanaofaa kushika nafasi muhimu kwenye serikali, nasaha hizo zikipuuzwa tatizo litaendelea kuwepo, hili ni jambo la wakuu ndio watakao beba lawama.

Akaongeza kua, watu wenye sifa zilizo tajwa na Marjaiyya wapo, wairaq wengi wanauwezo mkubwa ni wasafi na wana elimu, tatizo hawajapewa nafasi wala madaraka, mtu asiyekua na uwezo ndiye mwenye madaraka na maamuzi na mwenye uwezo hana madaraka wala maamuzi.

Kwa heshima yako naomba ushauri na nasaha zako kwetu, kwa sababu tutatakiwa kusaidia serikali mpya na kuhakikisha inakua serikali bora inayo wafaa wairaq, unatupa ushauri na nasaha gani kwa kutusaidia?

Umoja wa mataifa ni sawa na mwamvuli wa kimataifa hautakiwi kuegemea upande wowote, unatakiwa usaidie kutatua matatizo yaliyopo, nilipo kua Basra, alinijia mtu wa Yunesko kwa lengo la kutusaidia kutatua tatizo la maji, kwa hakika alitutumia mashine mbili za kusukuma maji, tulifanya kazi kwa sharti la kutoingiza mitazamo ya siasa, bila shaka Iraq inamatatizo makubwa katika sekta ya elimu na afya pia kuna mripuko wa maradhi, na tatizo la maji linaweza kuongezeka siku za mbele kama swala la maji halitapangiliwa vizuri bamoja na baadhi ya nchi za jirani, kuna matatizo mengine tunaweza kuyaita matatizo mpandano, kama kusipo kuwepo na kuaminiana yanaweza kusababisha vita, hasa itakapo kua –Allah atuepushe- vita ya kutumia siraha, itakua vigumu kuidhibiti, miongoni mwa jukumu la umoja wa mataifa ni kujenga kuaminiana kati ya makundi tofauti, ndio watanufaika wote na bila kuaminiana wote watapata hasara.

Baada ya mkutano huo ugeni ulitembelea makumbusho ya vifaa na nakala kale, wakafurahishwa sana na uwezo wa raia wa Iraq katika makumbusho hiyo iliyo anzishwa mwaka 2009m, na kutengeneza maeneo yake ya makumbusho pamoja na kuipangilia vizuri kwa namna ambayo inakidhi vigezo vya kimataifa, na kazi zote zinafanywa na watumishi wa makumbusho hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: