Toghuti ya ofisi ya wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaingia katika familia ya toghuti za mtandao wa kimataifa Alkafeel…

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umeingiza toghuti ya ofisi ya wanawake katika familia ya toghuti zake, itakua ni sawa na dirisha litakalo wawezesha watu wa ndani na nje ya Iraq kufuatilia habari zake.

Anuani ya toghuti hiyo ni: https://alkafeel.net/women_library/index.php

Nayo imesanifiwa na kupangiliwa na idara ya intanet ambayo ipo chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Ayabatu Abbasiyya tukufu, imepangiliwa kisasa kutokana na maendeleo ya Dunia katika sekta hiyo, ili iweze kuongeza uzuri katika mtandao wa kimataifa Alkafeel, watalamu wamechagua rangi nzuri zinazo endana na toghuti hiyo, pamoja na kuchagua upangiliaji bora wa milango yake, na wametumia njia bora zaidi ya kupangilia toghuti, na kuifanya kuwa rahisi zaidi katika utumiaji wake.

Toghuti hii inamilango kadhaa, miongoni mwa milango yake ni:

  • 1- Habari: unaelezea harakati za ofisi ya wanawake na mambo wanayo fanya.
  • 2- Maktaba ya picha za video: mlango huu unapicha za video zinazotengenezwa na ofisi ya wanawake, zinahusu mambo mbalimbali.
  • 3- Maktaba ya picha za mnato: mlango huu unapicha mbalimbali zinazo onyesha harakati za ofisi ya wanawake.
  • 4- Wewe ni kiigizo changu: mlango huu unaelezea wanawake watukufu katika historia ya kiislamu, na kuandika historia zao kwa ufupi.
  • 5- Tusome pamoja: mlango huu unamachapisho mbalimbali yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo mtu ataweza kujisomea kupitia mlango huu.
  • 6- Riyaadhu Zaharaa: ni tawi la toghuti ya jarida la (Riyaadhu Zaharaa) nalo ni jarida ambalo hutolewa kila mwezi na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 7- Matatizo: mlango huu unahusika na kurusha matukio ya kila mwezi yanayo tokana na idara ya msaada wa kusoma katika ofisi ya wanawake, ambapo yanaandikwa mambo yaliyo somwa na marafiki wa maktaba wanaosoma kwenye mtandao au kwa kuja moja kwa moja katika maktaba ya wanawake.
  • 8- Marafiki wa maktaba: mlango huu unalenga kushajihisha usomaji wa wanawake, kwa hiyo mwanamke anaye penda kushiriki anaweza kuchagua kitabu katika mlango huu, baada ya kumaliza kukisoma anatuandikia muhtasari wa alicho elewa katika kitabu hicho, muhtasari huo utagaguliwa na kamati maalumu ya majaji kisha tunaweza kuuweka katika mlango wa matatizo au mlango huu huu.

Fahamu kua toghuti hii inasimamiwa na wanawake walio bobea chini ya ofisi ya wanawake, na walipewa semina ya namna bora za kuingiza taarifa katika mtandao na kwenye kila mlango miongoni mwa milango yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: