Jumuiya ya Skaut yafanya matembezi ya kuomboleza na kukumbuka majonzi ya Ashura…

Maoni katika picha
Jumuiya ya Skaut ya Alkafeel chiniya ya idara ya watoto na makuzi ya Atabatu Abbasiyya tukufu wamefanya matembezi ya kuomboleza Alasiri ya Ijumaa ya leo (18 Muharam 1440h) sawa na (28 Septemba 2018m) karibu wanachama wa Skaut (200) wameshiriki katika matembezi hayo, kwa ajili ya kuomboleza kifo cha Imamu Hussein na watu wa nyumbani kwake (a.s) na maswahaba zake walio uwawa siku ya Ashura, na kujikumbusha misingi ya uislamu na ubinaadamu iliyo fundishwa na Bwana wa Mashahidi (a.s) na akakubali kumwagika damu yake takatifu.

Matembezi hayo ni sehemu ya ratiba ya Ashura iliyo andaliwa na jumuiya hiyo na kupewa jina la (Labbaika yaa Hussein), ratiba hiyo inaendelea hadi ziara ya Arubaini, hii ni kwa ajili ya kutengeneza kizazi cha watu wanao wapenda Ahlulbait (a.s) na kufuata mwenendo wao sahihi na kufahamu mambo yaliyo msibu Imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya kuibakiza na kuiendeleza dini ya kiislamu na sheria za Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Matembezi yalianzia katika eneo la mlango wa Bagdad wakaja hadi katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), wakipitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na yakaishia katika uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufanya majlis ya kuomboleza, majlis ilikua na vipengele mbalimbali, miongoni mwa vipengele vyake ni: usomaji wa Qur’an tukufu, usomaji wa khutuba ya Abulfadhil Abbasi (a.s) aliyoitoa siku ya Ashura, ambayo ilisomwa na mmoja wa wanajumuiya ya Skaut, pamoja na muhadhara ulio tolewa na Shekh Ahmadi Shawili ambaye ameongelea malengo ya harakati ya Imamu Hussein (a.s), majlis hii ilifungwa kwa kaswida zilizo somwa na Muhsin Salami na Muhammad Mahdi Asadiy.

Watembeaji walikua wamebeba mabango yaliyo andikwa ishara za msiba na mengine yalikua yameandikwa ujumbe wa kupinga dhulma na kuishi kwa amani na mengoneyo yanayo tokana na harakati ya Imamu Hussein (a.s), yakiwemo mabango yanayo himiza umoja, ubinadamu na kutafuta elimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: