Mradi mkubwa zaidi wa uandishi wa yaliyo tokea baada ya fatwa ya kujilinda umepiga hatua kubwa na wasimamizi wasisitiza kua ni safari ya milele…

Maoni katika picha
Mradi wa; kitabu cha fatwa tukufu ya kujilinda (Mausua fatwa difai Almuqaddasah) –ambao ni mradi mkubwa zaidi unaofanywa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu- umepiga hatua kubwa, baada ya watu walio pewa jukumu la kukusanya taarifa na kuandika kufikia karibu asilimia %98, mtandao wa kimataifa Alkafeel umeangalia hatua iliyo fikiwa na namna utendaji unavyo fanyika chini ya maelekezo ya kamati maalumu inayo simamia mradi huo.

Mradi huu ulianza kutekelezwa kwa ajili ya kutunza kazi kubwa na muhimu zilizo fanywa baada ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani kutoa fatwa tukufu ya kujilinda (Jihadi kifaya ya kujilinda), na namna fatwa hiyo ilivyo fanyiwa kazi na raia wa Iraq, walijitokeza kwa wingi na kuzuwia mashambulizi ya magaidi wa Daesh katika miji mingi ya Iraq, fatwa hiyo ilisaidia kuongeza uwezo wa askari na kuwatia moyo wapiganaji, jambo lililo wafanya waweze kupigana vita kali zaidi na hatimae wakaishinda nguvu ya ugaidi na upotevu.

Kitabu hiki kinaandikwa kwa baraka za Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu Ashrafu na kinazaidi ya juzuu kumi na mbili, kila juzuu lina vifungu kadhaa vinavyo elezea mambo yaliyo fanyika kutokana na fatwa tukufu na kuleta ushindi.

Katika juzuu la kwanza: kuna vifungu sita vinavyo elezea historia ya harakati ya kukufurishana (takfiriyya) na magenge ya kigaidi pamoja na harakati za salafiyya.

Na juzuu la pili: linazungumzia athari za Marjaa Dini mkuu na misimamo mashuhuri zaidi kitaifa, lina vifungu vitatu ambapo tumeangazia kipindi cha kuanzia mwaka (1914m) hadi (2003m).

Juzuu la tatu: lina vifungu vitatu, vinaelezea mazingira ya kijeshi baada ya mwaka (20014) na kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda pamoja na vipengele muhimu vilivyo zungumziwa katika khutuba ya Ijumaa.

Juzuu la nne: linaelezea juhudi zilizo fanywa na hauza za elimu katika mji wa Najafu, katika sekta ya kuwajenga wapiganaji kiimani na sekta ya kutoa misaada kwa wapiganaji, pia zilitoa wapiganaji, kuna kundi kubwa la mashahidi miongoni mwa watu wa dini na wanafunzi wa hauza.

Juzuu la tano: linaelezea juhudi zilizo fanywa na Ataba tukufu za Iraq na namna walivyo jitolea katika swala hilo.

Juzuu la sita: linaelezea namna vita hiyo ilivyo tangazwa katika vyombo vya habari vya kimataifa na vya kiarabu.

Juzuu la saba: linavifungu viwili, kifungu cha kwanza kinaelezea juhudi zilizo fanywa na mawakibu Husseiniyya na kifungu cha pili kinaelezea juhudi zilizo fanywa na taasisi za kiraia na za serikali, chini ya anuani isemayo: Misaada ya kimkakati na kibinaadamu ya raia.

Juzuu la nane: linaelezea mashahidi walio tokana na fatwa tukufu kwa ajili ya kutunza damu zao tukufu zilizo komboa taifa hili.

Juzuu la tisa: limeitwa (Fatwa tukufu katika macho ya watafiti na wana lugha), na linavifungu viwili, kifungu cha kwanza kinaelezea makala zilizo andikwa kufuatia fatwa tukufu, na kifungu cha pili kinaelezea mambo yaliyo andikwa kuhushu ushujaa wa wapiganaji kwa kuandika matukio halisi yaliyo tokea.

Majuzuu mengine yataendelea kuelezea uhalisia wa kipindi muhimu katika historia ya Iraq, na mambo makuu yaliyo shuhudiwa katika kipindi hicho, na tutamalizia kwa kuandika ushahidi wa kweli wa kihistoria.

Kamati inayo simamia mradi huu imesisitiza kua, mradi huu ni safari ya milele, inayo tunza historia isiharibiwe na kupotoshwa, na litakua kimbilio la kila anayetafuta ukweli, ili juhudi hizi zisipotee, Atabatu Abbasiyya tukufu imebeba jukumu la kihistoria la kuandika yote yaliyo tokea na kuyarithisha vizazi vijavyo yakiwa salama, ili waweze kuona kazi zilizo fanywa na wazazi wao na namna walivyo jitolea nafsi na mali zao, na namna Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu alivyo kua na uwezo wa kusimamisha haki na kuondoa batili, tunapenda kufahamisha kua kitabu hiki kimekusanya misimamo, ushujaa na matukio yaliyo fanyika Iraq na wananchi wa Iraq ambayo mtu anaweza kushindwa kuandika matukio mengine yanayo fanana na haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: